Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
HATIMA ya Michael Richard Wambura kugombea au kutogombea Urais wa klabu ya Simba SC itajulikana jioni ya leo, kufuatia jana kikao cha Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kumalizia kesi yake.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Julius Lugaziya ameiambia BIN ZUBEIRY asubuhi ya leo kwamba, jana walifanya kikao hadi Saa 4:30 usiku bila kumaliza na wamepanga kukutana tena leo kuanzia Saa 6:00 mchana kuendelea.
“Lakini tumefikia sehemu nzuri, tumewahoji pande zote mbili za wahusika wa rufaa, kwa maana ya mkata rufaa na wakatiwa rufaa. Leo tutaanzia kwenye kupitia maelezo yao na kisha kutoa maamuzi,” amesema Lugaziya, mmoja wa mawakili wanaoheshimika nchini.
Kamati ya Lugaziya ilikutana jana kuanzia Saa 5:00 asubuhi kwenye hoteli ya Courtyard, Upanga, Dar es Salaam kusikiliza rufani moja inayopinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba.
Michael Wambura amewasilisha rufani yake TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba iliyomwengua katika kinyang’anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

![]() |
Hatima ya Michael Wambura (mwenye suti katikati) inaweza kujulikana leo jioni baada ya Kamati ya Rufani kuhitimisha zoezi la kupitia kesi yake |
“Lakini tumefikia sehemu nzuri, tumewahoji pande zote mbili za wahusika wa rufaa, kwa maana ya mkata rufaa na wakatiwa rufaa. Leo tutaanzia kwenye kupitia maelezo yao na kisha kutoa maamuzi,” amesema Lugaziya, mmoja wa mawakili wanaoheshimika nchini.
Kamati ya Lugaziya ilikutana jana kuanzia Saa 5:00 asubuhi kwenye hoteli ya Courtyard, Upanga, Dar es Salaam kusikiliza rufani moja inayopinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba.
Michael Wambura amewasilisha rufani yake TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba iliyomwengua katika kinyang’anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment