UBELGIJI ina nafasi kubwa ya kuongoza kundi hili mbele ya Urusi, Korea Kusini na Algeria Kombe la Dunia mwaka huu.
BIN ZUBEIRY inakuletea hitimisho la uchambuzi wa beki wa zamani wa England, Martin Keown akimalizia na Kundi H.
Kund H
Ubelgiji
Korea Kusini
Algeria
Urusi
Utabiri wa Keown;
1 Ubelgiji
2 Urusi
3 Korea Kusini
4 Algeria
Ratiba (Saa za Afrika Mashariki)
Jun 17 Ubelgiji v Algeria Saa 1:00 usiku B. Horizonte
Jun 17 Urusi v Korea Kusini Saa 7:00 usiku Cuiaba
Jun 22 Ubelgiji v Urusi Saa 1:00 usiku R. Janeiro
Jun 22 South Korea v Algeria Saa 4:00 usiku P. Alegre
Jun 26 Korea Kusini v Ubelgiji Saa 5:00 usiku S. Paulo
Jun 26 Algeria v Urusi Saa 5:00 usiku Curitiba
Jun 17 Urusi v Korea Kusini Saa 7:00 usiku Cuiaba
Jun 22 Ubelgiji v Urusi Saa 1:00 usiku R. Janeiro
Jun 22 South Korea v Algeria Saa 4:00 usiku P. Alegre
Jun 26 Korea Kusini v Ubelgiji Saa 5:00 usiku S. Paulo
Jun 26 Algeria v Urusi Saa 5:00 usiku Curitiba
UBELGIJI
Viwango vya FIFA: Namba 11
Kocha: Marc Wilmots. Aliwahi kuwa mwanasiasa kwa muda na pia ni mchezaji wa mwisho kuifungia Ubelgiji katika Kombe la Dunia mwaka 2002.
Nahodha: Vincent Kompany (Man City)
Mchezaji wa kumulikwa: Eden Hazard (Chelsea). Ubelgiji ina wachezaji wengi wenye vipaji, lakini Hazard ni nyota. Ni wing wenye maarifa katika soka ya dunia ya leo, lakini sasa anahitaji kuithibitishia dunia uwezo wake katika michuano hiyo mikubwa.
Fuata ninayokuambia; Kocha wa Ubelgiji, Marc Wilmots akitoa maelekezo kwa Naodha Vincent Kompany
Ubora wao: Wanamiminika mbele. Wabelgiji wanatumia mfumo wa 4-2-3-1, lakini viungo wao washambuliaji watatuwanaruhusiwa kutembea kwa uhuru na kutengeneza nafasi.
Tatizo: Kusaidiana majukumu. Kikosi ni imara, lakini washambuliajin wao wameelekeza fikra zao kwenye mabao na hawawezi kusaidia ulinzi.
Watakwenda England? Thibaut Courtois atarejea Chelsea wakati Arsenal na Liverpool wanamfukuzia mshambuliaji kinda wa Lille, Divock Origi ambaye aliingizwa kikosini mwishoni kabisa.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Nafasi ya nne (1986)
Walivyofika hapa: Waliongoza kiulaini Kundi A Ulaya, pointi tisa mbele ya Croatia, tena bila kupoteza mechi, huku nyavu zikitikisika mara sita tu.
Je, wajua? Mwishoni mea Fainali zilizopita za Kombe la Dunia, Ubelgiji walikuwa wanashika nafasi ya 48 kwenye viwango vya FIFA. Wakati ratiba ilipotolewa kwa ajili za Fainali za mwaka 2014, Ubelgiji ilikuwa moja ya timu zilizopiga hatua kubwa, kwa kupanda hadi nafasi ya tano.
ALGERIA
Viwango vya FIFA: Namba 22
Kocha: Vahid Halilhodzic. Kocha huyo wa zamani wa PSG anatarajiwa kuifikisha mbali Algeria safari hii.
Nahodha: Madjid Bougherra (Lekhwiya)
Mchezaji wa kumulikwa: Islam Slimani (Sporting Lisbon). Mshambuliaji huyo mwenye nguvu ni hatari kweli anapokuwa mbele ya lango. Mabao ya Slimani yalikuwa na mchango mkubwa katika mechi za kufuzu na alifunga mara 10 katika mechi 19 za Algeria.
Ubora wao: Kuzuia mashambulizi ya wapinzani. Mafanikio yao katika hatua ya makundi yalitokana na uimara wa safu yao ya ulinzi.
Hatari: Hawafiki mbali. Algeria haijawahi kutoka kwenye hatua ya makundi na uzoefu unaweza kuwagharimu mwaka 2014.
Watakwenda England? Slimani anatakiwa na West Ham wakati Newcastle inamfuatilia winga Sofiane Feghouli wa Valencia.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Hatua ya makundi (1982, 1986 na 2010)
Walivyofika hapa: Waliongoza kiulaini kundi lao H bars la Afrika, lakini wakafuzu kwenda Brazil kwa faida ya mabao ya genii baada ya safe ya jumla ya 3-3 na Burkina Faso katika mechi ya mwisho wa mchujo.
Je, wajua? Timu hiyo inaitwa kwa nina la utani The Desert Foxes, ambayo si ajabu kupewa nina hilo kwa kuwa sehemu ya Algeria ni jangwa.
URUSI
Viwango vya FIFA: Namba 19
Kocha: Fabio Capello. Mtaliano huyo atasherehekea kutimiza miaka 68 siku moja baada ya Urudi kucheza na Korea Kusini.
Nahodha: Sergei Ignashevich (CSKA Moscow)
Mchezaji wa kumulikwa: Alexander Kerzhakov (Zenit St. Petersburg). Mfungaji huyo bora katika historia ya Ligi Kuu ya Urusi– amefunga mabao zaidi ya 200– amekuwa akifanya vizuri chini ya Capello na atakuwa mshambuliaji wao wa kwanza Brazil.
Ubora wao: Vigumu kuwapita. Wanacheza mfumo wa kigumu wa 4-2-3-1 na wanalazimisha kupasua gnome ya wapinzani.
Tatizo: Mawasiliano. Baadhi ya wachezaji inasemekana hawavutiwi na ufundishaji wa Capello hususan ratiba zake.
Watakwenda England? Alexander Kokorin wa Dinamo Moscow na Alan Dzagoev wa CSKA wote wanatakiwa na Arsenal na Tottenham, lakini hawatapatikana kwa bei rahisi.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Nafasi ya nne (1966 – kama Soviet Union)
Walivyofika hapa: Waliongoza kundi lao Ulaya, wakiizidi pointi moja Ureno na kufungwa mabao matano tu katika mechi 10.
Je, wajua? Capello ni kocha anayeshika nafasi ya tano kwa kulipwa mshahara mkubwa kwenye ulimwengu wa soka, na kocha wa timu ya taifa anayeongoza kulipwa vizuri. Mshahara wake wa mwaka Urusi ni Pauni Milioni 6.5.
KOREA KUSINI
Viwango vya FIFA: Namba 57
Kocha: Hong Myung-Bo. Ni mchezaji aliyeichezea mechi nyingi Korea Kusini, jumla ya mechi 136 na alikuwa Nahodha wao katika Fainali za mwaka 2002.
Nahodha: Lee Chung-Yong (Bolton)
Mchezaji wa kumulikwa: Son Heung Min (Bayer Leverkusen). Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akicheza kwa ubora wa hali ya juu wakati wote Bundesliga nanni tumaini la Korea. Anapenda kushambulia kutokea pembeni kushoto, lakini ana macho makali langoni mwa wapinzani.
Ubora wao: Wanacheza kwa ujanja. Korea wanatumia mfumo wa kigumu wa 4-2-3-1, lakini wanapofanya shambulizi la kushitukiza wanabadilika na kutumia 4-2-4, wakati mwingine mabeki wa pembeni wakiongeza idadi.
Tatizo: Ukuta wao uchochoro. Muunganiko wao wa safu ya ulinzi unatoa nafasi ya kupoteza mipira mingi ya juu.
Atakwenda England? Heung-Min ni nyota anayewatoa udenda Liverpool, Manchester City na Chelsea, ambaye thamani yake ni Pauni Milioni 10.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Nafasi ya nne (2002)
Walivyofika hapa: Waliongoza kundi lao la kwanza licha ya kufungwa na Lebanon kabla ya kwedna kushika nafasi ya pili katuka kundi la mwisho loa kufuzu mbele ya Uzbekistan kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Je, wajua? Kocha Myung-Bo alitajwa katika orodha ya Pele ya magwiji 100 wa soka walio hai mwaka 2004. Alikuwa miongoni mwa wachezaji wawili tu wa bara la Asia pamoja na Hidetoshi Nakata.
0 comments:
Post a Comment