// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LEOPARDS YAIPIGA 2-1 AS REAL, ETOILE YAIFUMUA 4-3 NKANA KOMBE LA SHIRIKISHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LEOPARDS YAIPIGA 2-1 AS REAL, ETOILE YAIFUMUA 4-3 NKANA KOMBE LA SHIRIKISHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, June 08, 2014

    LEOPARDS YAIPIGA 2-1 AS REAL, ETOILE YAIFUMUA 4-3 NKANA KOMBE LA SHIRIKISHO

    Na Mwandishi Wetu, BAMAKO
    BAO la dakika ya mwisho la Kader Bidimbou limeipa ushindi Leopards FC wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, AS Real mjini Bamako katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya Jumamosi.
    Cesaire Gandze alitangulia kuwafungia wageni dakika ya 10, kabla ya Ali Badra Sylla kuisawazishia timu ya Mali dakika ya 64.

    Leopards ilikuwa imecheza mechi moja kabla na kutoa sare ya 1-1 na ASEC Mimosas, wakati AS Real ilifungwa pia mechi ya kwanza mabao 2-1 na Coton Sport de Garoua.
    Ushindi huo unamaanisha timu ya Kongo inapanda nafasi ya pili kwa pointi zake nne, ikizidiwa mbili na vinara Coton Sport.
    Katika Kundi B, vigogo wa Tunisia, Etoile du Sahel walitoka nyuma mara mbili na kuifunga Nkana FC ya Zambia mabao 4-3 mjini Sousse.
    Mabingwa hao wa mwaka 2006 sasa wanafikisha pointi tano, moja zaidi ya Al Ahly ambao Jumapili watamenyana na Sewe Sport mjini Abidjan.
    Nkana wanaendelea kushika mkia Kundi B wakiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi tatu na ni lazima waifunge Etoile kwenye mchezo wa marudiano Julai 26 michuano hiyo itakapoendelea baada ya Kombe la Dunia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LEOPARDS YAIPIGA 2-1 AS REAL, ETOILE YAIFUMUA 4-3 NKANA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top