MSHINDI wa Ballon d'Or, Cristiano Ronaldo na timu yake ya Ureno wapo kundi moja na Ujerumani, Ghana na Marekani katika Kundi G Kombe la Dunia.
BIN ZUBEIRY inaendelea kukuletea makala za mchambuzi na beki wa zamani wa England, Martin Keown haps akilichambua Kundi G.
Kundi G
Ujerumani
Ureno
Marekani
Ghana
Utabiri wa Keown;
1 Ujerumani
2 Ureno
3 Marekani
4 Ghana
Ratiba (Saa za Afrika Mashariki)
Jun 16 Ujerumani v Ureno Saa 1:00 usiku Salvador
Jun 16 Ghana v Marekani Saa 7:00 usiku Natal
Jun 21 Ujerumani v Ghana Saa 4:00 usiku Fortaleza
Jun 22 Marekani v Ureno Saa 7:00 usiku Manaus
Jun 26 Marekani v Ujerumani Saa 1:00 usiku Recife
Jun 26 Ureno v Ghana Saa 1:00 usiku Brasilia
Jun 16 Ghana v Marekani Saa 7:00 usiku Natal
Jun 21 Ujerumani v Ghana Saa 4:00 usiku Fortaleza
Jun 22 Marekani v Ureno Saa 7:00 usiku Manaus
Jun 26 Marekani v Ujerumani Saa 1:00 usiku Recife
Jun 26 Ureno v Ghana Saa 1:00 usiku Brasilia
UJERUMANI
Viwango vya FIFA: Namba 2
Kocha: Joachim Low. Amesaidia mapinduzi makubwa ndani ya kikosi cha Ujerumani na sasa watu watapenda kujua atavuna nini.
Nahodha: Philipp Lahm (Bayern Munich)
Mchezaji wa kumulikwa: Thomas Muller (Bayern Munich). Alikuwa mchezaji bora chipukizi Fainali za mwaka 2010, lakini nilikuwa pembeni mwa Uwanja walipofungwa na Italia kwenye Euro 2012 na akawaka. Anahitaji kudhibiti hasira zake, kwa sababu ni mchezaji mzuri na tegemeo la timu.
Kivyake: Miroslav Klose ni mshambuliaji pekee halisi kikosi cha Ujerumani aliyekwenda Brazil
Ubora wao: Wanashambulia mno. Walifunga mabao 36 katika mechi za kufuzu, ambayo ni mengi kuliko timu coyote ya Ulaya. Wakiwa na viungo wengi wa kushambulia, unaweza kuona sababu ya kuvuna mabao mengi.
Tatizo: Kumalizia kazi wanashindwa. Tangu washinde Euro 96, Ujerumani imefika imefika fainali mbili za mashindano makubwa na Nusu Fainali tatu, lakini hakuna walichoonyesha.
Watakwenda England? Manchester United inamtaka nyota wa Dortmund, Mats Hummels na Bastian Schweinsteiger, ambaye Bayern wake tayari kumuuza. Marco Reus na Toni Kroos wanavutia timu pia England.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Washindi (1954, 1974 na 1990)
Walivyofika haps: Waliongoza kundi C katika mechi za kufuzu Ulaya wakishinda mechi tisa kati ya 10 walizocheza. Nyingine walitoa safe ya 4-4 na Sweden, mchezo ambao waliongoza 4-0.
Je, wajua: Ujerumani hawajapoteza mechi kwa mikwaju ya penalti kwa miaka 37 tangu walipofungwa na Czechoslovakia katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Ulaya mwaka 1976. Tangu waliposhinda mara tano katika mechi tano, mara mbili dhidi ya England.
URENO
Viwango vya FIFA: Namba 4
Kocha: Paulo Bento. Amejipatia nina la utani ‘Papa-tacas’ au ‘cup-eater’ alipokuwa Sporting Lisbon baada ya kushinda mataji manne.
Nahodha: Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
Mchezaji wa kumulikwa: Cristiano Ronaldo (Real Madrid). Unaweza kusema mini kuhusu Ureno bila kumtaja Ronaldo? Amekuwa akisumbuliwa na majeuthi kidogo siku za karibuni mwishoni mea msimu, lakini alithibitisha thamani yake kwa kufunga mabao yoto manne katika mechi ya mchujo dhidi ya Sweden Novemba mwaka jana. Tarajia mambo makubwa Brazil.
Mtu babu kubwa: Cristiano Ronaldo ni tumaini la Ureno Kombe la Dunia Brazil
Ubora wao: Kuwa bora nje ya Ronaldo - Mfumo mzima unamtegemea yeye. Wanatumia mfumo wa 4-3-3 kushambulia huku Ronaldo akiteleza pembeni kushoto.
Tatizo: Kuwa na mpango wa pili. Wanamtegemea sana Ronaldo, ambaye anapodhibitiwa au kukosekana timu nzima inapotea.
Watakwenda England? Fabio Coentrao anatakiwa Liverpool na Tottenham. Manchester United wanamtaka kiungo William Carvalho na Hugo Almeida anaweza kuhama bure baadaye.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Washindi wa 3 (1966)
Walivyofika hapa: Walishika nafasi ya pili nyuma ya Urusi kwenye kundi lao kabla ya kuifunga Sweden 4-2 katika mechi mbili za mchujo, mechi ya marudiano wakishinda 3-2 ugenini na kujitakia tiketi ya Brazil.
Je, wajua? Ronaldo ameshinda Ballon d’Or mwaka 2013, lakini mshindi huyo wa tuzo hiyo ya Mwanasoka Bora wa Dunia anakwenda Kombe la Dunia akiwa hajawahi kushinda taji la michuano hiyo
GHANA
Viwango vya FIFA: Namba 37
Kocha: Kwesi Appiah. Mwafrika mweusi wa kwanza kuiongoza Ghana Kombe la Dunia.
Nahodha: Asamoah Gyan (Al Ain)
Mchezaji wa kumulikwa: Emmanuel Agyemang Badu (Udinese). Kiungo huyo ana umri wa miaka 23 lakini tayari ameichezea timu yake ya taiga mechi zaidi ya 40. Akiwa na urefu wa futi 5 na inch 8 hana mwili mkubwa, lakini ni kiungo mahiri anayesambaza vyema mipira katika ya Uwanja na 'mapafu ya mbwa'.
Ubora wao: Wanakimbiza lie mbaya. Ghana wanapenda kucheza kwa kasi na hawahofii kupiga mipira mirefu pembeni kwa wachezaji wao wenye kasi kushambulia.
Hatari: Wanakaribisha kushambuliwa. Iwapo timu za wapinzani zinawapeleka kwa kasi mabeki wao, wanakosa ujanja wa kuidhibiti hali hiyo na kushambuliwa kwa urahisi.
Watakwenda England? Mshambuliaji Abdul Majeed Waris wa Valenciennes amekuwa akipigiwa hesabu na Leicester na Everton. Andre Ayew anatakiwa na Hull lakini anaweza kuwa ghali mno.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Robo Fainali (2010)
Walivyofika hapa: Waliongoza kundi lao kwa kushinda mechi tano kati ya sita kabla ya kuifunga Misri kwa jumla ya mabao 7-3 katika mechi mbili za mwisho za mchujo.
Je, wajua? Timu yao inajulikana kwa nina la utani ‘The Black Stars’ – katakana na bendera ya nchi yao, ambayo ina alama ya nyota nyeusi na kampuni ya zamani ya meli.
MAREKANI
Viwango vya FIFA: Namba 13
Kocha: Jurgen Klinsmann. Mjerumani huyo ameahidi kuimba nyimbo za mataifa yote, wakati Marekani itakapokutana na Ujerumani.
Nahodha: Clint Dempsey (Seattle Sounders)
Mchezaji wa kumulikwa: Michael Bradley (FC Toronto). Mchezaji huyo kivutio wa Marekani, alianza kucheza wakati baba yake Bob alipokuwa kocha, lakini akajipambanua kwenye ulimwengu wa soka kwa kuhamia Ulaya. Nguvu na utaalamu, vilimfanya acheze vyema Roma kabla ya kuhamia Toronto Januari.
Ubora wao: Hawaondoki kwenye mipango yao ya mchezo. Marekani haimuogopi coyote chini ya Klinsmann na inajaribu kuulazimisha mchezo wanavyotaka wao, lakini katika kundi lao maneno yatakuwa rahisi kuliko vitendo.
Ndoto ya Marekani: Lakini kocha wa Marekani, Jurgen Klinsmann lazima apambane na nchi yake Ujerumani katika hatua ya makundi
Tatizo: Kutumia mshambuliaji mmoja. Katika kundi gumu kama hili, kutumia washambuliaji wawili inaweza kusaidia, lakini kwa wao wanaotaka kutumia mtu mmoja watataabika.
Watakwenda England? Beki wa kati Matt Besler amekuwa akizungumziwa na timu kama Stoke, Crystal Palace, QPR na West Ham. John Anthony Brooks na Julian Green wanaweza kustaajabisha kidogo.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Washindi wa 3 (1930)
Walivyofika hapa: Waliongoza kundi katika hatua ya kwanza ya mchujo mbele ya Jamaica na wakafanya hivyo tena katika kundi la mwosho la CONCACAF, wakiizidi kwa pointi Costa Rica.
Je, wajua? Klinsmann alikaribia kushinda Kombe la Mabara mwaka 2009 akiwa na Marekani. Waliifunga Hispania 2-0 Nusu Fainali kabla ya kufungwa na Brazil 3-2 kwenye fainali licha ya kuongoza kwa mabao mawili.
0 comments:
Post a Comment