UFARANSA wanakwenda Brazil kiroho safi baada ya jana kuichapa Jamaica mabao 8-0 katika mchezo wa mwisho wa kujipima kabla ya kuanza kwa michuano hiyo wiki hii.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema alifunga mabao mawili, akapika mawili pia, la nne lililofungwa na Oliver Giroud na la pili lililofungwa na kiungo Blaise Matuidi. Mutuidi naye alimsetia Benzema bao lake la pili.
Winga nyota, Franck Ribery ameondolewa kwenye kikosi cha Ufaransa kwa sababu ya majeruhi, lakini bado Les Blues imeendelea kung'ara.
Shuti: Benzema alifunga mabao tote akiwa pembeni kwa boksi mkono wa kushoto
Giroud alimsetia bao la kwanza kiungo Yohan Cabaye, beki wa kushoto, Patrice Evra alimmiminia krosi Matuidi kufunga la pili usiku huo, na Antoine Griezmann alitokea benchi kufunga mabao mawili matamu.
Kiasi cha mwaka mmoja uliopita, Benzema alikuwa anasotea nafasi kikosi cha kwanza baada ya kucheza mechi 15 bila kufunga, lakini sasa amefunga mabao sita katika mechi sita zilizopita alizoichezea Ufaransa hivyo kufikisha junla ya mabao 21 katijka mechi zote 66 akiwa na jezi ya Les Blues.
Huu ulikuwa ushindi mkubwa wa kwanza wa Ufaransa tangu waifunge 10-0 Azerbaijan mwaka 1995.
0 comments:
Post a Comment