MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku anaweza kukowa mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia baada ya kuumia kifundo cha mguu akiiwezesha Ubelgiji kushinda 1-0 dhidi ya Tunisia mjini Brussels juzi.
Mpachika mabao huyo mwenye umri wa miaka 21 hatofanya mazoezi kwa siku nne, manna yake yuko shakani kucheza mechi ya kwanza ya Ubelgiji ya Kundi H dhidi ya Algeria Juni 17.
Mashabiki wa Ubelgiji kwa ujumla watakuwa na hofu kwa sababu tayari wamempoteza mshambuliaji wa Aston Villa, Christian Benteke katika kikosi cha Kombe la Dunia baada ya kuumia miezi miwili iliyopita, akimuacha Lukaku abaki mshambuliaji pekee wa kwanza.
0 comments:
Post a Comment