// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); JANUZAJ AAMUA KUBAKI MAN UNITED, ASEMA ANATAKA KUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA, UTAIFA AMUACHIA BABA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE JANUZAJ AAMUA KUBAKI MAN UNITED, ASEMA ANATAKA KUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA, UTAIFA AMUACHIA BABA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, October 18, 2013

    JANUZAJ AAMUA KUBAKI MAN UNITED, ASEMA ANATAKA KUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA, UTAIFA AMUACHIA BABA

    KINDA Adnan Januzaj amesema kwamba anataka kuongeza Mkataba kuendelea kucheza Manchester United.
    Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18, alifunga mabao mawili dhidi ya Sunderland katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu England kwa mabingwa hao watetezi na anatarajiwa kusaini Mkataba wa muda mrefu Old Trafford. 
    Mkataba wa sasa wa Januzaj unatarajiwa kumalizika Juni 2014 na vigogo wa Ulaya, Juventus na Barcelona wanataka saini ya kiungo huyo, lakini anatarajiwa kubaki United na kusaini Mkataba mpya.

    Tayari kubaki: Mchezaji wa Manchester United, Adnan Januzaj anataka kubaki katika klabu hiyo

    Atachezea nchi gani?

    KOSOVO: Asili ya baba yake, Abedin, aliyezaliwa Kosovo. Lakini Kosovo si mwanachama wa FIFA. 
    UBELGIJI: Alipozaliwa. Alizaliwa mjini Brussels na kuishi huko hadi alipotimkia Manchester. 
    ALBANIA: Ni kwa asili. Wazazi wake asili yao Albanian. 
    UTURUKI: Kwa ukoo. Babu zake ni Waturiki. 
    ENGLAND: Mhamiaji, ikiwa ataishi England kwa miaka mingine mitano atapewa uraia.
    "Nina furaha Manchester United na ninataka kujifunga kwa asilimia 100 kufanya vizuri katika kila mechi," Januzaj aliiambia Shirika Televisheni ya Kosovo, KTV.
    "Nataka kuisaidia Manchester United kushinda ubinga wa Ligi Kuu na kuwa mchezaji bora duniani,".
    Mustakabali wa soka ya kimataifa bado haueleweki kwa Januzaj, pamoja na hayo kinda huyo haruhusiwi kuichezea England hadi awe ameishi kwa miaka mitano nchini humo.
    Amekwishaishi England kwa miaka miwili, hivyo atalazimika kusubiri hadi mwaka 2016.
    "Ni baba yangu anayemua nichezee timu gani ya taifa, nitachezea atakapoamua, hivyo nitamsikiliza yeye,"alisema Januzaj.
    Aiming for the top: Januzaj says he wants to become the best player in the world
    Anataka kuwa matawi ya juu: Januzaj amesema anataka kuwa mchezaji bora duniani
    In the goals: Januzaj scored twice for United against Sunderland
    Mkali wa maba: Januzaj aliifungia mabao mawili United dhidi ya Sunderland
    Staying put: Januzaj looks set to stay at Manchester United
    Anabaki: Januzaj anatarajiwa kubaki Manchester United
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JANUZAJ AAMUA KUBAKI MAN UNITED, ASEMA ANATAKA KUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA, UTAIFA AMUACHIA BABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top