• HABARI MPYA

    Sunday, March 03, 2013

    JAMHURI NJE AFRIKA, SIMBA WASHALALA 1-0, AZAM WANAONGOZA 2-0 SUDAN

    Kipre Tchetche amewafunga tena Nasir

    Na Waandishi Wetu
    JAMHURI ya Pemba, imekuwa timu ya kwanza ya Tanzania kuaga michuano ya Afrika, baada ya kufungwa mabao 5-0 na wenyeji Kedus Giorgis nchini Ethiopia katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Matokeo hayao, yanamaanisha, Jamhuri imeaga kwa kufungwa jumla ya mabao 8-0, baada ya awali kutandikwa 3-0 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Gombani, Pemba.
    Wawakilishi wengine wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC hadi mapumziko walikuwa nyuma kwa bao 1-0 mbele ya wenyeji Recreativo de Libolo mjini Calulo nchini Angola, bao lililofungwa dakika ya 10 tu.
    Hali hiyo inazidi kuwaweka mguu nje Simba SC katika michuano hiyo, kufuatia awali kufungwa pia 1-0 nyumbani.
    Simba inacheza vizuri, lakini Recreativo wanautumia zaidi upande wa kushoto ambao ni dhaifu hii leo, anakocheza Amir Maftah kushambulia.
    Na hata bao lilitokana na Maftah kuzembea kuokoa mpira hadi mfungaji akaingiza mguu kutokea nyuma yake na kufunga.
    Wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, Azam FC wao wanaendelea vyema, hadi sasa wakiwa wanaongoza mabao 2-0 ugenini Sudan, dhidi ya wenyeji Al Nasir Juba.
    Mabao hayo yamefungwa kipindi cha kwanza yote na washambuliaji ‘mwiba’ wa Azam, Kipre Herman Tchetche la kwanza na John Raphael Bocco ‘Adebayor’ la pili. Azam ilishinda 3-1 katika mechi ya kwanza Dar es Salaam. Matokeo kamili yatawajia baada ya mechi hizo kumalizika.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: JAMHURI NJE AFRIKA, SIMBA WASHALALA 1-0, AZAM WANAONGOZA 2-0 SUDAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top