• HABARI MPYA

    Wednesday, November 07, 2012

    AZAM KUJIULIZA KWA JKT OLJORO LEO CHAMAZI

    Azam FC

    Na Prince Akbar
    LIGI Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi tatu za viporo kuchezwa kwenye viwanja vitatu tofauti.
    Wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Simba, Mtibwa Sugar leo wataikaribisha JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
    Coastal Union nao watashuka kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kumenyana na Polisi Morogoro, huo ukiwa mchezo wa kwanza tangu wafungwe mabao 4-1 na Azam wiki iliyopita
    Azam FC, wakiwa na kumbukumbu ya kutandikwa mabao 2-0 tena wakichezewa soka ambayo hawajawahi kuiona kwa timu nyingine yoyote ya Tanzania, wao watakuwa kwenye Uwanja wao wa Chamazi, kumenyana na JKT Oljoro
    Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi, Mgambo JKT ikimenyena na Azam FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, African Lyon na Mtibwa Sugar Chamazi, Dar es Salaam, Simba SC na Toto Africans Taifa, Dar es Salaam, Prisons na JKT Ruvu Sokoine, Mbeya, Kagera Sugar na Polisi Morogoro, Kaitaba, Bukoba na JKT Oljoro na Ruvu Shooting Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
    Mechi nyingine ya kuhitimisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu itachezwa Jumapili, Yanga wakiwa wageni wa Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanfa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM KUJIULIZA KWA JKT OLJORO LEO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top