![]() |
| La Myia |
MSANII La'Myia, mzaliwa wa Panorama City,
California mtoto wa Tyra Doyle na Leon Good, ameiambia bongostaz.blogspot.com kwamba ametoa wimbo mpya.
Amejitambulisha kama dada wa mwigizaji Meagan Good na mpwa
wa mwimbaji na mwigizaji Dijon Talton.
Mwaka 2001, alitoa wimbo Good akiwa na LeTecia Harrison,
Ardena Clark na Quierra Davis-Martin ambao walianzisha kundi la R&B lililoitwa
Isyss.
Wakiwa kama kundi mwaka 2002 walitoa albamu "The Way We
Do", ambayo ilijumuisha nyimbo zilizoingia kwenye chati za Hot 100 kama
"Day & Night" waliomshirikisha rapa Jadakiss na "Single For
The Rest Of My Life". Wamewahi kuingizwa kwenye kinyang’anyiro cha tuzo mbili
za Soul Train Lady of Soul na walishinda tuzo moja.
Bahati mbaya walipigwa chini na lebo ya Arista Records kutokana
na mauzo mabaya ya albamu yao kabla hawajatoa albamu yao ya pili.
Albamu yao pekee "The Way We Do" ilishika namba 55
katika chati za Billboard na kuuza nakala 300,000.
Baada ya kuachana na kundi hilo mwaka 2006, Good na
"Love" wote walijiunga na kundi jipya la R&B, lililojulikana kama
BAD GYRL.
Mwaka 2011 aliimba wimbo Speak Wit Ur Body wa AY wa Tanzania, ambao alimshirikisha pia Good na
Romeo Miller.
Mwaka 2012 alitoa wimbo wake mpya ulioitwa Graduate Me akimshirikisha
Tyga (Young Money Cash Money Brother).
Good pia ni mwigizaji na ameshiriki show mbalimbalin za TV
kama Tall Hopes, Sister, Sister, The Parent 'Hood, Smart Guy, ER, The Parkers na
Judging Amy.
Pia amecheza filamu kama The Wood na Busted iliyotoka karibuni.



.png)
0 comments:
Post a Comment