• HABARI MPYA

    Thursday, April 19, 2012

    NDUGU YAKE MESSI KUTUA MAN UNITED, ATARAJIWA KUTISHA MBAYA

    Gaitan
    KOCHA Msaidizi wa zamani wa Manchester United, Carlos Quieroz anaamini winga wa Benfica, Nicolas Gaitan ana nafasi kubwa ya kujenga jina katika Ligi Kuu ya England.
    Gaitan, ambaye alijiunga na Benfica akitokea Boca Juniors majira ya joto 2010, alipiga mzigo wa uhakika katika mechi zote mbili za timu yake ya Manchester United katika Ligi ya Mabingwa msimu huu.
    Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye anaweza kucheza kama kiungo mshambuliaji au winga wa kushoto, sasa imeelzwa anawaniwa na kocha wa Mashetani Wekundu, Sir Alex Ferguson.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Argentina, nchi anayotoka Mwanasoka Bora wa Dunia, Lionel Messi anaweza kuuzwa kwa pauni Milioni 38 kulingana na mkataba wake wa sasa Estadio da Luz, lakini taarifa zimesema uhamisho wake kwenda England utakamilika mwishoni mwa msimu.
    Inaaminika kwamba Gaitan atakwenda Old Trafford kwa dau la pauni Milioni 20, na beki wa pembeni wa Brazil, Fabio na mshambuliaji Mtaliano, Federico Macheda watajiunga na Benfica kwa mkopo wa muda mrefu, huku mpango wa kuhamia huko moja kwa moja ukisukwa.
    Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59, Quieroz, kwa sasa ni Kocha Mkuu wa Iran na hana shaka juu ya uwezo wa Gaitan kumpa maisha bora England.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDUGU YAKE MESSI KUTUA MAN UNITED, ATARAJIWA KUTISHA MBAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top