• HABARI MPYA

    Thursday, April 19, 2012

    SUDAN WAWASILI KUWAVAA AKINA ULIMWENGU KESHOKUTWA

    TIMU ya taifa ya Sudan chini ya umri wa miaka 20, (U20) inawasili leo saa 7.25 mchana (Aprili 19 mwaka huu) kwa ndege ya Ethiopian Airlines namba ET 805 ikiwa na msafara wa watu 30.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura, ameiambia bongostaz.blogspot.com hivi punde kwamba Sudan inatarajiwa kufikia kwenye hoteli ya Rungwe iliyoko eneo la Kariakoo, Dar es Salaam. Timu hiyo imepangiwa kufanya mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Karume, na kesho itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa.
    Wambura amesema vilevile kesho saa 4 asubuhi kutakuwa na mkutano wa makocha wa Tanzania U20 na Sudan U20 na Waandishi wa Habari saa 4 kamili asubuhi ofisi za TFF.
    Mechi hiyo, itachezeshwa na marefa kutoka Uganda Jumamosi Uwanja wa Taifa.
    Refa atakayechezesha mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Brian Miiro na wasaidizi ni Mark Ssonko na Lee Patabali wakati mwamuzi wa mezani ni Denis Batte wakati kamisaa ni Ejigu Ashenafi kutoka Ethiopia.
    Kamisaa na waamuzi hao pia wanawasili nchini leo kwa ndege za Ethiopian Airlines na Air Uganda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUDAN WAWASILI KUWAVAA AKINA ULIMWENGU KESHOKUTWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top