| Marehemu Rutta |
MWILI wa mjumbe wa
kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga Theonest Rutashoborwa (pichani)unatarajiwa
kuagwa jumatatu ijayo katika kanisa katoliki parokia ya kijichi kabla ya
kusafirishwa kwenda kwao kijiji cha Bukabaye kilicopo Bukoba mkoani
Kagera.
Kwa mujibu wa mamapipiro.blogspot, Rutashoborwa ambaye
kitaaluma ni wakili akimiliki kampuni ya Brilliance Law Chambers ya jijini Dar
es Salaam alikutwa na umauti huo usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Agha
Khan alipokwenda baaada ya kujisikia vibaya kabla ya kubainika kuwa na kisukari
na shinikizo la damu.
Ofisa habari wa
Yanga, Louis Sendeu amesema kuwa Rutashoborwa alianza kujisikia vibaya mara
alipotua uwanja wa ndege wa mwalimu Jk Nyerere akitokea Moshi, Kilimanjaro
alipokwenda kwa shughuli zake za kikazi na alipokimbizwa hoispitalini alifariki
akiwa katika harakati za kupelekwa chumba cha uangalizi maalum
(ICU).
“Yanga inasikitisha
kumpoteza kiongozi huyu hidari ambaye alikuwa muhimili mkuu katika kuinganisha Yanga,
kwa nianba ya wanachama na wapenzi wa Yanga tunatoa pole kwa familia ya
marehemu, ndugu jamaa na marafiki,”Alisema Sendeu.
“Marehemu ameacha
mjane na watoto wanne, bwana ametoa Bwana ametwaa, mwenyezi mungu aiweke rioho
ya marehemu mahali pema peponi, Amin,”Alisema.
Rutashoborwa atakumbukwa sana Yanga, kutokana na jitihada zake zilizosaidia klabu hiyo kumpata mfadhili, Yussuf Manji mwaka 2006.


.png)
0 comments:
Post a Comment