![]() |
| Di Matteo |
KAIMU kocha wa Chelsea, Roberto
Di Matteo amesema leo kwamba yanahitajika mabadiliko katika hatua za kinidhamu
zinazochukuliwa na Chama cha Soka England (FA), baada ya klabu yake kupata pigo
kwa mchezaji wake, Branislav Ivanovic kuadhibiwa.
Di Matteo anaamini FA ilikosea kumtia
hatiani Ivanovic kwa kumchezea rafu kiungo wa Wigan, Shaun Maloney, wakati
mshambuliaji wa Manchester City, Mario Balotelli hakuadhibiwa kwa kumchezea
rafu Alex Song wa Arsenal.
Ivanovic amefungiwa mechi tatu, na
ataikosa Nusu Fainali ya Kombe la FA Jumapili dhidi ya Tottenham, baada ya FA
kutumia udhahidi wa video kumtia hatiani beki huyo wa Serbia.
Di Matteo anashawishika kwamba
taratibu za FA hazina uhakika wanapochukua uamuzi ambao unaziathiri klabu.
"Nafkiri kila mtu anatazamia
maamuzi ya uhakika kutoka FA. Hicho ndio muhimu kwa kila mtu, wadau wote
wakiwemo - uhakika," alisema.
"Wangerudia maamuzi wanayotoa
na adhabu wanazotoa, na ni matumaini kwamba wangekuja na maamuzi ya usawa zaidi."alisema.
Di Matteo pia alitaka ushahidi
wa video utumike kwa mapama marefu zaidi, akitolea mfano wa tukio la Ivanovic:
"Unaangalia katika picha na unafikiri: 'Tunatumia picha za video kwa hilo,
sawa, lakini kwa nini hatukutumia teknolojia ya kwenye goli'.
"Kwa nini hapana? Kama tumetumia
hii kwa ajili ya hilo, kwa nini tusitumie hiyo kwa mabao? Hivyo, ni kwa nini
inapaswa kutazamwa upya (taratibu za adhabu za FA). Inatakiwa kuwa ya haki zaidi
na usawa.



.png)
0 comments:
Post a Comment