![]() |
| Asia kulia, Sharifa kushoto walipokuwa na Kanumba katikati Marekani Januari mwaka jana |
MBUNIFU wa mavazi nchini Asia
Idarous ambaye kwa sasa yuko Marekani, amedai kushtushwa sana na msiba wa
msanii Steven Kanumba.
Akizungumza na bongostaz kutoka Marekani, Asia alisema ameshitushwa sana na msiba
huo.
Pamoja na kushitushwa huko, pia
ameelezwa kuhuzunishwa na kukosa nafasi ya kuja nchini kuhudhuria mazishi yake.
Akielezea jinsi alivyopokea
taarifa hizo, Asia alisema alikuwa katika moja ya maonyesho yake Mjini Dallas
na hivi karibuni na wakati anatoka nje ya ukumbi akadokezwa kuwa Kanumba
amefariki.
“Nilikuwa kwenye onyesho langu
la Lady In Redy nchini Marekani na wakati natoka nje nikapewa taarifa hizo za
msiba, kiukweli imeniumiza sana kwa kuwa Kanumba alikuwa kama mwanangu,” alisema
Asia.
+na+Sharifa+walipokutana+na+marehemu+Steven+Kanumba,+Washington+DC+nchini+Marekani+Januari+mwaka+jana.jpg)


.png)
0 comments:
Post a Comment