• HABARI MPYA

    Thursday, November 10, 2016

    BIN KLEB: SHEIKH SAID ALIPIGANIA UMOJA WA KLABU

    Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb amesema kwamba atamkumbuka Sheikh Said Muhammad Abeid kwa mchango wake mkubwa katika kuunda umoja wa klabu Tanzania.
    Sheikh Said aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC na makamu Mwenyekiti wa Bosi ya Ligi alifariki dunia Jumatatu jioni na kuzikwa Jumanne katika makaburi ya Kisutu, jirani na msikiti wa Maamour, Upanga ambako mwili wake ulisaliwa baada ya sala ya Alasiri.
    Na Bin Kleb alisema juzi wakati wa mazishi kwenye makaburi Kisutu kwamba watamkumbuka Sheikh Said kwa mchango wake katika kuanzisha umoja wa klabu, ambayo matunda yake ni kuzaliwa kwa Bodi ya Ligi. 
    Abdallah Bin Kleb amesema kwamba atamkumbuka Sheikh Said Muhammad Abeid kwa mchango wake mkubwa katika kuunda umoja wa klabu Tanzania

    “Tulikuwa naye bega kwa bega wakati mimi nipo Yanga pale katika kuanzisha umoja wa klabu, ambao matunda yake ni ujio wa Bodi ya Ligi, ambayo yeye alikuwa ni Makamu wake,”alisema.
    Mwenyekiti wa makampuni ya Bakhresa Group, wamili wa Azam FC, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa alihudhuria mazishi hayo pamoja na wanawe wakiwemo, Mkurugenzi Mkuu wa makampuni hayo, Abubakar.
    Sura za viongozi wa klabu na vyama mbalimbali vya michezo nchini, wanachama maarufu wa klabu za soka na wafanyakazi wa makampuni mbalimbali ya Bakhresa Group wakiwemo wachezaji wa timun za vijana na Azam ndizo zilizotawala wakati wa mazishi hayo.
    Sheikh Said Muhammad Abeid enzi za uhaiwake akiwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

    Wachezaji wa kikosi cha kwanza chab Azam FC hawakuwepo kwa sababu wapo na timu hiyo Mwadui, Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na wenyeji, Mwadui kesho.  
    Sheikh Said alizaliwa Machi 20 mwaka 1940 visiwani Zanzibar na anatarajiwa na enzi za ujana wake alicheza soka na Kriketi. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Sheikh Said Muhammad Abeid mahali pema peponi, Amin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BIN KLEB: SHEIKH SAID ALIPIGANIA UMOJA WA KLABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top