• HABARI MPYA

  Wednesday, October 12, 2016

  YANGA NA MTIBWA UHURU, SIMBA NA MBEYA CITY SOKOINE LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA watetezi, Yanga SC leo watakuwa wanatafuta ushindi wa kwanza ndani ya mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakati mahasimu wao, SImba SC watakuwa mjini Mbeya kupigania kuendela kubaki kileleni.  
  Yanga watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kusaka ushindi ikitoka kufungwa 1-0 na Stand United na sare ya 1-1 na Simba SC.
  Vinara wa Ligi Kuu, Simba SC watakuwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kumenyana na wenyeji, Mbeya City katika mchezo mwingine wa ligi hiyo wakisaka pointi za kuendelea kuwaweka kileleni. 
  Michezo mingine itakayopigwa kesho; Majimaji itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.
  Stand United itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga na katika mkoa huo huo Mwadui itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye dimba la Mwadui Complex huku timu pinzani za Mwanza ‘Mwanza Derby’ kati ya Mbao na Toto Africans itapigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo. Alhamisi Oktoba 13, 2016 Ruvu Shooting itacheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Mabatini.
  Simba SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 17, ilizovuna kwenye mechi saba, ikifuatiwa na Stand United yenye pointi 16 za mechi nane, Mtibwa Sugar pointi 14 za mechi nane, Mbeya City pointi 12 za mechi nane, wakati Yanga SC yenye pointi 11 za mechi sita, ni ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA MTIBWA UHURU, SIMBA NA MBEYA CITY SOKOINE LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top