• HABARI MPYA

  Monday, October 17, 2016

  NYASI ZA BANDIA ZA NYAMAGANA ZAWASILI TFF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  HATIMAYE nyasi za bandia za kuweka kwenye Uwanja wa mkongwe wa Nyamagana mjini Mwanza zimewasili ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imeelezwa.
  Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas Mapunda amesema leo katika mahojiano na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba nyasi hizo zilizokuwa zimezuiwa kwa takriban mwaka mzima kwa sababu ya ushuru, tayari wamezipokea.
  “Hivi ninavyozungumza na wewe hapa, tayari kontena mbili za nyasi bandia na vifaa vyake vyote zipo hapa makao makuu ya TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na wakati wowote zitasafirishwa kwenda Mwanza,”amesema. 
  Ofisa Habari huyo wa TFF, amesema kwamba kwa sasa wanasubiriwa wataalamu tu kutoka China au Ujerumani ili waende kuzitandika nyasi hizo bandia mjini Mwanza.
  Katika hatua nyingine, Mapunda alisema kwamba Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limatoa taarifa ya ujio wake kuja kukagua Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza pia, ili kuupitisha tena kwa matumizi ya michezo ya kimataifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NYASI ZA BANDIA ZA NYAMAGANA ZAWASILI TFF Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top