• HABARI MPYA

    Monday, May 25, 2020

    MCHEZAJI NA KIONGOZI WA ZAMANI WA YANGA SC AFARIKI DUNIA LEO HOSPITALI YA MUHIMBILI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BEKI wa zamani wa klabu ya Yanga, Lawrcence Mwalusako amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Muhimbli alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
    Kwa mujibu wa mjomba wa marehemu, Augustino Mwakyembe – Mwalusako ambaye pia alichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars miaka ya 1980 alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya Kiharusi. 
    Msiba wa Mwalusako aliyewahi pia kuwa Katibu wa Yanga SC kwa awamu tofauti upo nyumbani kwake, Kimara Jijini Dar es Salaam na taarifa zaidi zinatarajiwa kutolewa na familia ya marehemu.
    Pumzika kwa amani; Lawrence Mwalusako (kushoto) akimkaabidh Ngassa aliposaini kurejea Jangwani Mei 20, mwaka 2013 akitokea kwa mahasimu, Simba SC alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka Azam FC
      
    Mwalusako alijiunga na Yanga SC mwaka 1985 akitokea Pan Africans iliyomuibua akiwa bado mwanafunzo wa sekondari.
    Akiwa Yanga SC, Mwalusako aliyekuwa anacheza nafasi zote za ulinzi pembeni kulia na kushoto pamoja na katikati, alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na akacheza hadi mwaka 1990 alipoamua kustaafu.
    Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Lawrence Mwalusako.

    Tutakukumbuka daima; Lawrence Mwalusako (kulia) akiwa na mshambuliaji Abeid Mziba enzi zao wanacheza Yanga SC mwaka 1987
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHEZAJI NA KIONGOZI WA ZAMANI WA YANGA SC AFARIKI DUNIA LEO HOSPITALI YA MUHIMBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top