• HABARI MPYA

    Sunday, May 17, 2020

    WAKATI UMEFIKA MGOGORO WA ZFF NA TFF UPATIWE SULUHU

    Na Ibrah Mkemia, DAR ES SALAAM
    ILIKUWA jioni moja hivi ambayo ilikuwa tulivu sana mandhari ya mji wenye raha tele ikiwa imechanganyika na sauti za wafanya biashara zikiendelea kuita wateja kufika katika biashara zao.  Siku hiyo nilikuwa natoka zangu katika harakati za kutafuta riziki ili mkono uweze kwenda kinywani.
    Nikapita sehemu ambayo nilikuta watu wamekusanyika kwenye kijiwe. Kutokana na uchovu wa safari na tabu ya usafiri wa dar es salaam nikajikuta najumuika katika kijiwe hiko na kuweza kupata walau kikombe kimoja cha sharubati ya miwa. Kama wasawahili wanavyosema "kawia ufike" na "kwenye wengi kuna mengi" stori zilikuwa zinaendelea za hapa na pale. Sijui ilikuwa ni ugeni wangu wa kijiwe au uchovu wa safari. 
    Ila nilijikuta nimetulia mithili ya maji mtungini nikisikiliza maongezi ambayo yalikuwa yamejaa mafunzo na utani mwingi. Moja ya mada ambazo zilikuwa zikizungumzwa ni kuhusu mgao ambao shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limepokea kutoka kwa shirikisho la soka duniani FIFA. Ili kuweza kuendesha miradi mbalimbali nchini hasa katika nyanja ya soka la vijana, wanawake na timu za taifa.
    Nyota wa Zanzibar anayecheza Ligi Kuu ya Bara, Feisal Salum wa Yanga akimtoka kiungo mwenzake, Mzambia Clatous Chama wa Simba SC. Zanzibar inaweza kuibua vipaji vingi zaidi kama itawezeshwa na TFF

    Kwenye kile kijiwe kulikuwa na mtu ambae alikuwa kama kiongozi wa sehemu ile kwa maana ya muendesha mada amabaye alikuwa anaruhusu mtu kuweza kuchangia mada. Mikono mingi ilinyooshwa ili watu waweze kutoa hoja zao kuhusiana na mada hiyo moyoni nikasema "Tanzania yetu hii mmh kila mtu mjuaji" basi watu walitoa yao ya moyoni walizungumza walikumbushia mambo mbalimbali ilimradi tu basi ni story za kijiweni.
    Nilitamani kuchangia ila kutokana muda na kufikiria zaidi usafiri nikanyanyuka na kulipia Sharubati niliyokunywa kisha nikaondoka iyo sehemu.  Lakin nikiwa barabarani jasho lililosababishwa na sharubati niliyokunywa likiendelea kinimiminika nikajikuta nakumbuka yale malalamiko kutoka kwa viongozi wa ZFA dhidi ya TFF kuhusu mgao huo . nikajiuliza maswali mengi sana kichwani ila nikakosa jibu.
    Kuna muda inabidi busara zitumike ili mambo kama haya yaweze kupatiwa ufumbuzi kuna mambo TFF na ZFA mnayafumbia macho kuyajadili. Migogoro hii imeibuka mara kadhaa sasa na muafaka bado haujapatikana kwangu nahisi ni kwa sababu ya utambuzi katika mashirikisho ya soka husika ambayo ni FIFA na CAF.
    Hapa naona kila sekta inatambua mwanachama wake kwa eneo lake na hii ndo shida ambayo inaleta mgongano kati ya shirikisho la soka Tanzania TFF na chama cha mpira wa miguu Zanzibar ZFA. Ikimbukwe ikija  kesi ya FIFA basi Tanzania bara na visiwani inakuwa kitu kimoja lakini kwa CAF basi hapo kuna na nchi mbili ambazo zinajitegemea. Huu ndo mkanganyiko uliopo kwa sasa.
    Je kuna misingi yoyote ambayo imewekwa kisoka kupelekea kuondoa sintofahamu na mkanganyiko kiutendaji. Kuna vitu vingi vinawatenganisha isifikie hatua mpaka kati yenu ikatokea kunakuwa na ugumu wa kimaamuzi. Kwani hakuna chombo cha juu cha kuwaweka pamoja kati ya TFF na ZFA.
    Sio vibaya kukumbuka mazuri ya waasisi wa nchi hii ambao walifanya makubwa sana na pongezi kwao ambao ni Mwalimu Nyerere na Mzee Karume kuweza kuonganisha pande zote mbili na hatime kupata nchi moja ya Tanzania. 
    Kuanza kutofautiana kwa sababu ya fedha kutoka kwa mashirikisho ya soka ni kuwakosea hshima na adabu wazee hawa waliotutangulia mbele ya haki kwani hatujui walifikiria nini mpaka wakaamua kuunga hizi pande mbili.
    Kiukweli tufike mahali kugombania misaada ya FIFA na CAF ifike mwisho ni aibu kwa taifa pia tunazipa tabu wizara zetu kuona jambo hili ni kubwa ambalo lihame katika mambo ya soka na kuanza kijadiliwa kisiasa. Kwani waliofanya muungano walitambua kuwa tutaungana kwa kila kitu hadi katika maswala ya michezo na ndio maana kulikuwa na ligi ya muungano. Hii yote ni kiashiria kuwa sisi ni wamoja na letu wote ni moja.
    Tusifikie hatua ya kuvunja amani ya muungano kwa kupokea misaada kutoka kwa mashirikisho ya soka. Tukae tujiulize tunafanyaje kama taifa kuhakikisha tunapiga hatua moja mbele kimpira ili kuwa nchi yenye mafanikio makubwa sana duniani.
    Ni wakati sasa wa kupata viongozi ambao watakuwa kati ya TFF na ZFA ili kupata muafaka pindi mambo kama haya yanapojitokeza. Kuwe na kanuni kama leo hii ZFA itapata kuwa mwanachama wa FIFA basi itwezaje kujiondoa ubavuni mwa TFF. Haya ndo mambo ambayo tunataka kuyasikia sio kila siku pesa za mashirikisho zije kuharibu amani ya muungano wetu 
    Zanzibar na Tanganyika mtoto wao ni Tanzania tusijimwambafai tukapoteza maana halisi ya jina hilo. Tuendelee kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa hatari wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona.
    (Imeandikwa na ibrah mkemia | kalomoibrahim@gmail.com | 0715147449/069294532
    @mkemia_tza)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAKATI UMEFIKA MGOGORO WA ZFF NA TFF UPATIWE SULUHU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top