• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 11, 2020

  MSHAMBULIAJI MGHANA, MICHAEL SARPONG AKIRI KUWA KWENYE MIPANGO YA KUJIUNGA NA YANGA SC

  Na Canisius Kagabo, KIGALI
  MSHAMBULIAJI Mghana aliyeachana na Rayon Sports ya Rwanda, Michael Sarpong amekubali kufuatwa na Yanga, lakini amesema hajafanya uamuzi.
  Mwishoni mwezi uliopita, Rayon Sports ilifukuza starika huu kwa ajili ya kukosa nidhamu, ni baada ya kusema maneno alikasirikisha kamati ya timu.
  Wakati alikuwa akidai kulipwa mshahara alisema kwamba rais wa timu hana uwezo wa kuongoza timu.
  Baada ya hapo ndipo habari nyingi zilisambaa mitandaoni na kusema Yanga ilitafuta njia zote za kumusajilia.
  Akizungumza na Bin Zubeiry – Sports Online, Michael Sarpong alikubali kwamba Yanga iko miongoni mwa timu zinazomhitaji.

  Michael Sarpong amekubali kufuatwa na Yanga, lakini amesema hajafanya uamuzi

  “Ndiyo, Yanga walinikaribia tukazungumza lakina sijachakua uamuzi. Nina ofa nyingi, napaswa kwanza nitulie tutafanya mambo kwa utulivu. Wakala wangu atamaliza kazi.”
  Michael Sarpong alitua Rwanda 2018. Alianza kuchezea Rayon Sports tangu Octoba 2018, alisaidia Rayon Sports kushinda kombe la ligi msimu uliopita a 2018-2019.
  Wakati huo huo, kiungo Mkongo wa Rayon Sports, Kakule Mugheni Fabrice amekanusha madai kwamba anataka kuhamia Yanga.
  Siku zilizopita, magazeti mbali mbali yaliripoti kwamba kijana huyo, ambaye yuko mwishoni mwa mkataba wake kwenye klabu ya Rayon Sports alianza mazungumzo na Young Africans ili msimu ujao akuje Jangwani.
  Kakule Mugheni Fabrice, kupitia ukuta wake wa Instagram, alikanusha madai hayo akisema ni uongo na akafichua kwamba ameanza mazungumzo na Rayon Sports kwa kuendeleza mkataba wake.
  "Hayo ni uongo. Bado nina mkataba wa Rayon Sports ambao utamalizika siku chache, muda wake katika siku chache, tayari tumeshajadili uwezekano wa kuongezaa mkataba. Katika siku zijazo mtajua kama nitabaki hapa au kama nitabadilisha timu. " Kakule alisema
  2018 Kakule alijiunga na Rayon Sports kutoka Kiyovu Sports, ambapo alikuwa ameishi kwa mwaka mmoja, na alikuwa amejiunga na Kiyovu Sports baada ya kuacana na Rayon Sports.

  Kakule Mugheni Fabrice amekanusha madai kwamba anataka kuhamia Yanga
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSHAMBULIAJI MGHANA, MICHAEL SARPONG AKIRI KUWA KWENYE MIPANGO YA KUJIUNGA NA YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top