• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 01, 2020

  WINGA MGHANA WA YANGA SC, BERNARD MORRISON AWASHAURI MAKOCHA KUSAJILI WACHEZAJI WATAKAOIONGEZEA MAKALI TIMU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WINGA Mghana wa Yanga SC, Bernard Morrison ameshauri Uongozi wa Yanga na Benchi la ufundi kufanya usajili mzuri utakaoongeza thamani kwenye kikosi ili kujenga Yanga itakayotwaa mataji ya ndani na nje ya nchi pamoja na kutingisha kwenye michuano mbalimbali.
  Kwa mujibu wa tovuti ya Yanga, Morrison amesema japo hawezi kushauri moja kwa moja nani na nani wasajiliwe, lakini angependa kuona wanaongezeka wachezaji watakaoleta tija kwenye kikosi.
  "Kikosi sio kibaya, lakini tunahitaji maboresho, naamini Uongozi na benchi la ufundi wanayaona zaidi maeneo ya kuboresha. Natamani tuwe na kikosi tishio baada ya usajili," anasema.

  Anasema amekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga ili walau katika kipindi hicho aweke historia ya kutwaa mataji akiwa na Yanga ambayo anasema ni timu yenye hadhi na thamani kubwa sana Tanzania na Afrika.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WINGA MGHANA WA YANGA SC, BERNARD MORRISON AWASHAURI MAKOCHA KUSAJILI WACHEZAJI WATAKAOIONGEZEA MAKALI TIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top