• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 29, 2020

  SIMBA NA YANGA ZINAWEZA KUKUTANA TENA NUSU FAINALI YA AZAM SPORTS FEDERATION CUP

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  VIGOGO, Simba na Yanga wanaweza kukutana kwa mara ya tatu msimu iwapo watavuka hatua ya Robo ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Hiyo ni baada ya ratiba ya Robo Fainali na Nusu Fainali ya michuano hiyo kupangwa leo katika studio za Azam TV, wadhamini wa michuano hiyo zilizopo Tabata Jijini Dar es Salaam. 
  Simba SC watakutana na mabingwa watetezi, Azam FC na Yanga SC watamenyana na Kagera Sugar katika Robo Fainali wote wakiwa nyumbani na vigogo hao wakishinda watakutana baina yao kwenye Nusu Fainali.

  Robo Fainali nyingine zitakuwa ni kati ya Namungo FC dhidi ya Alliance FC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi na Sahare All Stars dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na washindi wa mechi hizo watakutana Nusu Fainali.
  Meneja Mashindano wa TFF, Baraka Kizuguto aliyeongoza droo hiyo akisaidiwa na wachezaji wa zamani, beki wa zamani wa Simba SC Boniphace Pawasa na kiungo wa zamani wa Yanga, Deo Lucas amesema kwamba fainali itapigwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.
  Mechi mbili za awali msimu huu, timu hizo zilitoka sare ya 2-2 Januari 4 na Machi 8 Yanga SC ilishiinda 1-0, bao pekee la kiungo Mghana, Bernard Morrison dakika ya 44.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA ZINAWEZA KUKUTANA TENA NUSU FAINALI YA AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top