• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 01, 2020

  MDAU MKUBWA WA SOKA YA WANAWAKE NCHINI, DK MANENO TAMBA AFARIKI DUNIA NA KUZIKWA LEO DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MDAU mkubwa wa soka ya wanawake nchini, Alhaji Dk. Maneno Tamba amefariki dunia mapema leo na kuzikwa jioni katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.
  Tamba ambaye pia alikuwa mmoja wa viongozi katika safu mpya ya timu ya Wanawake ya Yanga Princess amefariki leo katika hospitali ya Amana, Ilala Jijini Dar es Salaam alipokuw aamelazwa kwa matibabu.
  Klabu ya Yanga imesema omepokea kwa masikito makubwa taarifa za kifo cha Dk. Tamba ambaye mbali na kuwa Mwanachama wao wa muda mrefu, lakini pia alikuwa mdau mkubwa wa michezo hapa nchini ambaye ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya soka, hasa upande wa soka la Wanawake.
  Marehemu Dk. Tamba alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kuanzisha timu za wanawake ambapo alianzisha timu ya Sayari na baadaye Mburahati Queen ambazo zote alizihudumia na zilileta chachu kubwa katika soka la Wanawake hapa nchini.
  Allah akupe kauli thabit, mpendwa wetu Dk. Maneno Tamba

  "Tumempoteza kiongozi mahiri kwenye soka, tutamkumbuka sana na tutakumbuka mchango wake mkubwa kwenye maendeleo ya soka la wanawake, na katika klabu yetu. Yanga tumepata pigo sana kwa sasa maana alikuwa mmoja wa viongozi kwenye safu timu yetu ya wanawake, Yanga Princess na alikuwa na maono makubwa ya kuivusha timu yetu ya wanawake,"amesema Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla.
  Aidha uongozi wa Yanga unatoa pole kwa Familia ya Dkt. Tamba na wadau wa soka kote nchini kwa kuondokewa na kiongozi huyo muhimu katika maendeleo ya mchezo wa soka. Alhaj Dkt. Tamba amezikwa leo, tarehe 5 Mei 2020, katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla ametangaza kuahirishwa kwa Mkutano Mkuu wa klabu ya Yanga ambao ulipangwa kufanyika Mwezi Mei mwaka huu.
  Katika taarifa yake kwa Wanachama, Wapenzi na mashabiki wa klabu ya Yanga, Dkt. Msolla amesema Kamati ya Utendaji imefikia uamuzi huo kutokana na hali ya sasa ya uwepo wa ugonjwa wa Corona ambao umeathiri shughuli nyingi Duniani kote.
  Amesema kwa kuwa kuna maelekezo ya serikali kuzuia mikusanyiko, wameona ni vyema kuahirisha mkutano huo ikiwa ni kutii maagizo ya serikali lakini pia kuchukua tahadhari ya kuwalinda wanachama wa klabu ya Yanga na jamii kwa ujumla dhidi ya janga hili.
  Tarehe ya mkutano huo itatangazwa hapo baadaye hali hii ikitengemaa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MDAU MKUBWA WA SOKA YA WANAWAKE NCHINI, DK MANENO TAMBA AFARIKI DUNIA NA KUZIKWA LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top