• HABARI MPYA

    Friday, May 12, 2017

    RASMI, SPORTPESA NDIYO WADHAMINI WAKUU WA SIMBA SC

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya SportPesa Tanzania rasmi leo imetangza udhamini wake wa miaka mitano kwa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, wenye thamani ya Sh. Bilioni 4.96.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Mkurugezi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema kwamba wameingia mkataba huko kwa dhumuni la kuendeleza soka nchini na kuisaidia klabu ya Simba kufikia malengo yake.
    Akifafanua, Tarimba ambaye ni Mwenyekiti wa zamani wa mahasimu wa Simba, Yanga alisema kwamba, katika mkataba wao kwa mwaka wa kwanza wadhamini hao watatoa Sh. Milioni 888 na miaka itakayofuata wataongeza asilimia 5 na miaka miwili ya mwisho watatoa Sh. Bilioni 1 na kwamba fedha hizo zitatolewa kwa awamu nne kwa mwaka.


    Mtendaji Mkuu wa SportPesa Tanzania, Pavel Slavkov (kulia) akimkabidhi jezi mpya Rais wa Simba SC, Evans Aveva (katikati) jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuashiria kuanza rasmi kwa udhamini wa kampuni hiyo katika klabu hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas.

    Tarimba alisema kwamba Simba watapaswa kuyathibitisha matumizi ya fedha hizo kwamba yalifanyika kwa maendeleo ya soka.
    Alisema licha ya mkataba huo, pia kutakuwa na motisha klabu hiyo ikishinda mataji, mfano kwa ubingwa wa Ligi Kuu watapewa zawadi ya Sh. Milioni 100.
    “Pia ikishinda michuano kama (Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati) Kombe la Kagame pia watapewa zawadi na wakifanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika watapata zawadi ya Milioni. 250,”alisema Tarimba.
    Kwa upande wake, Rais wa Simba, Evance Elieza Aveva alisema kwamba mkataba huo utakuwa chachu kubwa ya kutimiza azma ya kufanya vizuri kwa klabu hiyo kuanzia sasa.
    “Huu udhamini utaifanya Simba ifanye vizuri ndani na nje, pia utatoa fursa ya maendeleo ya soka la vijana," alisema Aveva.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RASMI, SPORTPESA NDIYO WADHAMINI WAKUU WA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top