• HABARI MPYA

    Saturday, April 08, 2017

    HOSSAM HASSAN APANIA KUWAZIMA KCCA LEO KWAO KAMPALA

    GWIJI wa Misri, ambaye sasa ni kocha wa El Masry, Hossam Hassan anaamini anaweza kuwazima wenyeji Kampala City Council Authority (KCCA) katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika leo mjini Kampala.
    Hossam ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online jana mjini Kampala kwamba licha ya kuwa taarifa chache za wapinzani wao, wapo hapaa kwa ajili ya kushinda kuelekea mchezo wa marudiano.
    “Tumekuja kufuata matokeo mazuri Kampala ambayo itafanya mchezo wetu wa marudiano uwe mwepesi,” amesema Hossam, ambaye ni kati ya ndugu wawili maarufu waliovuma kwenye soka ya Misri, kaka yake, Ibrahim ni Mkurugenzi wa Ufundi wa timu hiyo.
    Kocha wa El Masry, Hossam Hassan (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wake wa Ufundi na kaka yake, Ibrahim Hassan 

    Mkongwe huyo wa umri wa miaka 50, si mgeni wa soka ya Afrika akiwa ameshinda mataji kibao na vigogo wa Misri, Al Ahly na Zamalek na amesema KCCA ni timu madhubuti Uganda, lakini timu yake itacheza kiufundi kupata matokeo mazuri wanayotaka. 
    Wachezaji wawili tegemeo, Ahmed Shoukry na Ahmed Gomaa aliyefunga katika ushindi wa 2-0 wa Masry dhidi ya ENPPI kwenye Ligi Kuu ya Misri Jumapili iliyopita, pia wamesafiri na timu hiyo.
    Wakati Masry ni ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Misri, wenyeji wao, KCCA walipanda hadi nafasi ya pili kwenye Ligi ya Ugandan Jumanne iliyopita baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Bright Stars.
    Mabingwa wa Uganda walitolewa na mabingwa wa Afrika, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 kwenye hatua ya 32 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Kocha wa KCCA, Mike Mutebi, amesema hawawezi kuwatukuza wapinzani wao kutoka Misri. “Tunafahamu aina ya soka yao, ambayo ni kupiga pasi ndefu, lakini tunajua pa kuwakamatia,”alisema.
    Pamoja na hayo, Waganda hao watamkosa beki tegemeo, Joseph Ochaya, aliyejiunga na Lusaka Dynamos yab Zambia wiki mbili zilizopita.

    RATIBA MECHU ZAMCHUKO WA KUWANIA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO
    Leo, Jumamosi Aprili 8, 2017
    CF Mounana (Gabon) vs ASEC Mimosas (Ivory Coast)
    Bidvest (Afrika Kusini) vs Smouha (Misri)
    CNaPS (Madagascar) vs Recreativo do Libolo (Angola)
    KCCA (Uganda) vs El Masry (Misri)
    Yanga SC (Tanzania) vs MC Alger (Algeria)
    Jumapili Aprili 9, 2017
    FUS Rabat (Morocco) vs MAS Fes (Morocco)
    Rangers (Nigeria) vs Zesco (Zambia)
    RC Kadiogo (Burkina Faso) vs CS Sfaxien (Tunisia)
    Ports Authority (Gambia) vs Hilal Obeid (Sudan)
    Port Louis (Mauritius) vs Club Africain (Tunisia)
    Barrack Young Controllers (Liberia) vs Supersport (Afrika Kusini)
    AS Tanda (Ivory Coast) vs Platinum Stars (Afrika Kusini)
    Horoya (Guinea) vs Ittihad Tangier (Morocco)
    AC Leopards (Kongo) vs Mbabane Swallows (Swaziland)
    TP Mazembe (DRC) vs JS Kabylie (Algeria) 
    Jumamosi Aprili 15, 2017
    Rivers United (Nigeria) vs Rayon Sports (Rwanda)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HOSSAM HASSAN APANIA KUWAZIMA KCCA LEO KWAO KAMPALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top