• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 27, 2017

  SAMATTA AGONGA ZOTE 90 KRC GRNK, YATOA SARE 1-1

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amecheza dakika zote 90 usiku wa Jumatano, timu yake, KRC Genk ikilazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, AS Eupen Uwanja wa Kehrweg mjini Eupen katika mchezo wa Kundi B kuwania tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Europa League mwakani.
  Na Genk wenyewe ndiyo waliotangulia kwa bao la kiungo wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy dakika ya 19 kabla ya wenyeji kuchomoa kwa mkwaju wa penalti wa Luis Garcia dakika ya 51.
  Samatta alianza leo baada ya mchezo uliopita wa michuano hiyo kutokea benchi Jumapili Genk wakishinda 6-0 dhidi ya Royal Excel Mouscron nyumbani Uwanja wa Luminus Arena. 
  Genk inaendelea kuongoza Kundi B katika mchuano wa kuwania tiketi ya Europa League kwa pointi zake 13 sasa baada ya kucheza mechi tano.
  Samatta leo ameiichezea Genk mechi ya 54 tangu ajiunge nayo Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya DRC akiwa amefunga mabao 18.
  Kati ya mechi hizo 54, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 36 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 33 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 23 msimu huu.
  Mechi 20 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 12 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 18, 12 amefunga msimu huu na sita msimu uliopita.
  Kikosi cha KAS Eupen kilikuwa: From Crombrugge, Diallo, Al-Abdul Rahman, Diagne, Garcia, Bruls/Jeffren dk88, Sylla, Onyekuru, George/Timmermans dk90, Ocansey/Wague dk80 na Hackenberg.
  KRC Genk: Ryan, Uronen, Colley, Dewaest, Walsh, Berge, Malinovskyi/Heynen dk66 Pozuelo/Writers dk53 Trossard, Boetius/Naranjo 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AGONGA ZOTE 90 KRC GRNK, YATOA SARE 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top