• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 22, 2017

  MAN UNITED YATHIBITISHA ROJO NA ZLATAN WAMEMALIZA MSIMU

  Marcos Rojo pia ameumia goti katika mechi dhidi ya Anderlecht Alhamisi na atakosekana kwa sehemu yote ya msimu iliyobaki PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  TAKWIMU ZA IBRAHIMOVIC MSIMU WA 2016-2017 

  MECHI - 46
  MABAO - 28
  PASI ZA MABAO - 9
  NAFASI ALIZOTENGENEZA - 88 
  TIMU ya Manchester United itamalizia msimu bila wachezaji wake wawili tegemeo, beki Marcos Rojo na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic baada ya kuthibitishwa wameumia magoti. 
  Habari hizo ni pigo kubwa kwa United inayopigania taji dogo la Ulaya, Europa League na kumaliza ndani ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.
  Nyota wa Sweden, Ibrahimovic amefunga mabao 28 katika msimu wake wa kwanza kwenye soka ya England wakati Rojo amefanikiwa kuwa beki wa kati chaguo la kwanza mbele ya kocha Mreno, Jose Mourinho.
  Taarifa ya klabu leo Jumamosi imesema kwamba uchunguzi wa kina juu ya maumivu ya Marcos Rojo na Zlatan Ibrahimovic katika mchezo wa Europa League Alhamisi umethibitisha maumivu ya goti waliyopata wachezaji wote ni makubwa na watakuwa nje kwa muda mrefu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATHIBITISHA ROJO NA ZLATAN WAMEMALIZA MSIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top