• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 26, 2017

  YUSSUF MHILU AINUSURU YANGA B KULALA DODOMA

  Na Steven Kinabo, DODOMA
  TIMU ya vijana ya Yanga, maarufu kama Yanga B leo imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1
  Na wenyeji, Kombaini ya Majeshi Dodoma katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
  Timu hiyo ya Yanga B inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo, Nsajigwa Shadrack ‘Fusso’ ilicheza soka ya kuvutia na kuwafurahisha mashabiki waliojitokeza wakiwemo Wabunge na Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
  Yussuf Mhilu ameifungia Yanga bao la kusawazisha Dodoma leo ikitoa sare ya 1-1 na Kombaini ya Majeshi

  Hata hivyo, Yanga B ililazimika kupigana kusaka bao la kusawazisha baada ya wenyeji wao kutanguliwa kwa bao la Juma Yussuf dakika ya 43 kipindi cha kwanza bao hilo limedumu hadi kipindi cha kwanza kumalizika.
  Na iliwachukua Yanga hadi kipindi cha pili kupata bao la kusawazisha kupitia kwa kiungo wake, Yussuf Mhilu ambaye tayari ameanza kukomazwa kikosi cha kwanza aliyefunga bao hilo dakika ya 53.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YUSSUF MHILU AINUSURU YANGA B KULALA DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top