• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 20, 2017

  PRISONS WATAMBA KUWATUPA NJE YANGA KOMBE LA TFF

  Na Steven Kinabo, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa Prisons ya Mbeya, Abdallah Mohammed ‘Bares’ amesema kwamba wataing’oa Yanga katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana kwenye mazoezi ya timu yake Ukonga, Dar es Salaam, Bares alisema kwamba wamedhamiria kuchukua Kombe la TFF, maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Wachezaji wa Prisons wakifanya mazoezi Ukonga mjini Dar es Salaam jana

  “Tumejipanga kikamilifu kwa ajili ya mchezo huu, tayari tupo Dar es Salaam na tumekuwa kambini kwetu Ukonga tukijifua vikali kwa ajili ya mechi hii na lengo letu ni ushindi,”alisema Bares. 
  Alisema wanawaheshimu Yanga SC kama timu kubwa na mabingwa wa Tanzania, hivyo wanajua mchezo utakuwa mgumu, lakini watajitahidi kupigania ushindi.
  “Kitu ambacho najivunia tu ni kwamba vijana wangu wapo vizuri kuelekea mchezo huu na wana morali ya hali ya juu,”alisema.
  Yanga watakuwa wenyeji wa Prisons Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa Robo Fainali ya Kombe la ASFC kutafuta tiketi ya kuungana na Simba, Azam FC na Mbao FC ambazo tayari zimetinga Nusu Fainali ya michuano hiyo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PRISONS WATAMBA KUWATUPA NJE YANGA KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top