• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 21, 2017

  NI MAN UNITED NA WABABE WA SAMATTA NUSU FAINALI ULAYA


  NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE  

  Ajax vs Lyon
  Celta Vigo vs Manchester United
  Mechi za kwanza zitachezwa Mei 4 na marudiano yatakuwa Mei 11.
  TIMU ya Manchester United ya England itamenyana na Celta Vigo ya Hispania katika Nusu Fainali Europa League.
  Kikosi cha Jose Mourinho kitaanzia ugenini mechi ya kwanza Uwanja wa Balaidos Mei 4 na marudiano yatafuatia Old Trafford Mei 11.
  Katika Nusu Fainali nyingine, Ajax ya Uholanzi itamenyana na Lyon ya Ufaransa na mchezo wa kwanza utafanyika Amsterdam.
  Man United haijawahi kukutana na timu hiyo ya Hispania hapo kabla kwenye mashindano yoyote, lakini wanajiona bora kuliko Celta iliyo katikati ya msimamo wa La Liga.
  Celta Vigo ndiyo imehitimisha safari ya Nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta katika michuano ya Ulaya baada ya kuifunga KRC Genk kwa jumla ya mabao 4-3 wakishinda 3-2 kwenye mchezo wa kwanza Hispania kabla ya kulazimisha sare ya 1-1 usiku wa jana Uwanja wa Luminus Arena katika mchezo wa marudiano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI MAN UNITED NA WABABE WA SAMATTA NUSU FAINALI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top