• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 28, 2017

  SIMBA NA YANGA WACHUKUA TAHADHARI KUBWA DHIDI YA AZAM, MBAO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  VIGOGO wa soka nchini, Simba wameonekana kuchukua tahadhari kubwa kuelekea mechi zao za Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Mara tu baada ya kutangazwa kwa droo ya mechi za Nusu Fainali Jumapili iliyopita, mabingwa watetezi Yanga wakipelekwa Mwanza kwa Mbao FC na Simba wakibaki Dar es Salaam kwa ajili ya Azam FC vigogo hao walichukua hatua za mapema.
  Simba walipeleka kikosi chao kambini Morogoro kwa maandalizi ya kina wakati Yanga walifanya mchakato wa usafiri wa ndege kwenda Mwanza.
  Na baada ya kufika Mwanza jana jioni, Yanga walikwenda moja kwa moja Geita kuweka kambi fupi ya maandalizi hoteli ya Luns kabla ya kurejea mjini humo kesho.
  Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba kikosi cha kimejichimbia Geita na leo kimefanya mazoezi Uwanja wa Shule ya Msingi Waja.
  Hafidh amesema kikosi kitaondoka Geita kesho kurejea Mwanza tayari kwa mchezo huo wa Jumapili jioni Uwanja wa CCM Kirumba.
  Kwa upande wao, Simba SC wanatarajiwa kurejea Dar es Salaam leo tayari kwa Nusu Fainali ya kwanza kesho jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA WACHUKUA TAHADHARI KUBWA DHIDI YA AZAM, MBAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top