• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 22, 2017

  SERENGETI BOYS ‘YAWATAFUNA’ GABON 2-1 MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, RABAT
  TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo imeifunga Gabon mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki mjini Rabat, Morocco.
  Asante kwa wafungaji wa mabao hayo, Kelvin Nashon Naftali dakika ya 18 na Ibrahim Abdallah Ally dakika ya 75.
  Serengeti Boys imeweka kambi ya mwezi mmoja nchini Morocco kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, zinazotarajiwa kuanza Mei 14 hadi 28, mwaka huu nchini Gabon.
  Wachezaji wa Serengeti Boys na Gabon kabla ya mchezo wa leo
  Huo unakuwa mchezo wa nne wa maandalizi kwa Serengeti kujiandaa fainali za Gabon, baada ya kuifunga Burundi mara mbili, Machi 30 mabao 3-0 na Aprili 1 mabao 2-0, mechi zote mbili zikipigwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Ghana ‘Black Starlets’ Aprili 3 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Serengeti Boys itakuwa kambini mjini Rabat hadi Mei 1, mwaka huu itakapowenda Younde, Cameroon kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya wenyeji Mei 3 na 6, mwaka huu.
  Mei 7 timu hiyo itakwenda Gabon ambako imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola, wakati Kundi A lina timu za wenyeji, Gabon, Guinea, Cameroon na Ghana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS ‘YAWATAFUNA’ GABON 2-1 MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top