• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 21, 2017

  NI REAL NA ATLETICO MADRID, JUVE NA MONACO NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA
  NUSU FAINALI LIFI YA MABINGWA ULAYA  

  Real Madrid vs Atletico Madrid 
  Mechi ya kwnaza: Mei 2. Marudiano: Mei 9 
  Monaco vs Juventus 
  Mechi ya kwanza: Mei 3. Marudiano: Mei 10 
  WAPINZANI wa jiji la Madrid, Real Madrid na Atletico Madrid watakutana katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
  Nusu fainali nyingine itakuwa kati ya Juventus ya Italia na Monaco. 
  Katika marudio ya fainali ya msimu uliopita, mahasimu hao wa La Liga watakutana Uwanja wa Bernabeu Mei 2 na mchezo wa marudiano utafanyika Uwanja wa Vicente Calderon.
  Monaco watakuwa wenyeji wa mabingwa wa Serie A, Juventus Uwanja wa Louis II Mei 3 kabla ya kusafiri kwenda Turin kwa mchezo wa marudiano Mei 10. 
  Uwanja wa Cardiff ndiyo utakaohodhi fainali ya michuano hiyo Juni 3, hiyo ikiwa mara ya kwanza mfalme wa Ligi ya Mabingwa anapatikana katika ardhi ya Wales. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI REAL NA ATLETICO MADRID, JUVE NA MONACO NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top