• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 27, 2017

  NGOMA, BOSSOU KUIKOSA YANGA NA MBAO MWANZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI 22 wa Yanga SC wanatarajiwa kupanda ndege jioni ya leo kwenda Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sporrs Federation (ASFC) dhidi ya wenyeji, Mbao FC utakaofanyika Jumapili Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
  Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amewataja wachezaji wanaotarajiwa kuondoka ni makipa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Benno Kakolanya na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Oscar Joshua, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Hassan Kessy, Kevin Yondan, Andrew Vincent na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
  Donald Ngoma (kulia) atakosekana kwenye mchezo wa Jumapili kwa sababu ni majeruhi

  Viungo ni Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Said Juma ‘Makapu’, Juma Mahadhi, Simon Msuva, Geoffrey Mwashiuya, Obrey Chirwa na Emmanuel Martin wakati washambuliaji ni Amissi Tambwe na Matheo Antony.
  Wachezaji wanne watakosekana beki Vincent Bossou, kiungo Yussuf Mhilu na washambuliaji Malimi Busungu na Donald Ngoma.
  Bossou, Ngoma na Busungu ni majeruhi, wakati Mhilu yupo na kikosi cha timu ya vijana cha timu hiyo, ambacho jana kilitoa sare ya 1-1 na Kombaini ya timu ya Majeshi mjini Dodoma.    
  Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la ASFC inatarajiwa kuchezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Azam FC na Simba SC.
  Ikumbukwe Yanga SC ndiyo mabingwa watetezi wa Kombe la TFF baada ya kuifunga Azam 3-0 katika fainali mwaka jana. 
  Mara tu baada ya mchezo huo, Yanga inatarajiwa kurejea Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Prisons ya Mbeya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGOMA, BOSSOU KUIKOSA YANGA NA MBAO MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top