• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 26, 2017

  MAN UNITED KUMKOSA PAUL POGBA KESHO DHIDI YA MAN CITY

  Paul Pogba ataukosa mchezo wa mahasimu wa Jiji la Manchester Uwanja wa Etihad kesho kwa sababu ya majeruhi PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  ORODHA YA MAJERUHI MANCHESTER UNITED 

  Zlatan Ibrahimovic (goti)
  Marcos Rojo (goti)
  Juan Mata (nyonga)
  Chris Smalling (goti)
  Phil Jones (dole gumba) 
  Paul Pogba (nyama za paja) 
  KIUNGO Paul Pogba atakosekana katika mchezo wa kesho baina ya mahasimu wa Jiji la Manchester.
  Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema leo mchana kwamba kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa hajapona maumivu ya nyama za paja hivyo hatacheza dhidi ya mahasimu, City Uwanja wa Etihad Alhamisi.
  United watasafiri umbali mfupi wakijua kwamba ushindi utawapandisha juu ya majirani zao kwa mara ya kwanza tangu Agosti na kuingia ndani ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
  Lakini Mourinho atawakosa wachezaji kadhaa tegemeo akiwemo Pogba, Zlatan Ibrahimovic, Chris Smalling, Phil Jones, Marcos Rojo na Juan Mata.
  Kocha huyo wa United alisema; "Pogba? Hapana. Valencia pekee (anaweza kucheza). Tutakwenda na tulichonacho, tutapigana kwa tulichonacho. Nawaamini vijana. Wako tayari,".
  United ilishinda mechi ya ligi dhidi ya Burnley mwishoni mwa wiki bila wachezaji tegemeo na baada ya hapo, Mourinho akawapa changamoto nyota kama Smalling na Jones kujitahiid kucheza pamoja na maumivu, ingawa hakuna beki aliyefanya hivyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED KUMKOSA PAUL POGBA KESHO DHIDI YA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top