• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 26, 2017

  SAMATTA KAZINI NA GENK YAKE LEO UBELGIJI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo anatarajiwa kuiongoza klabu yake, KRC Genk katika mchezo wa Kundi B kuwania tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Europa League dhidi ya wenyeji, AS Eupen Uwanja wa Kehrweg mjini Eupen.
  Samatta anatarajiwa kuanza leo baada ya mchezo uliopita wa michuano hiyo kutokea benchi Jumapili Genk wakishinda 6-0 dhidi ya Royal Excel Mouscron nyumbani Uwanja wa Luminus Arena. 
  Genk inaongoza Kundi B katika mchuano wa kuwania tiketi ya Europa League kwa pointi zake 12 za mechi nne na imepania kupata nafasi ya kushiriki tena michuano hiyo ya Ulaya mwakani, baada ya mwaka huu kuishia Robo Fainali ambako walitolewa na Celta Vigo ya Hispania wiki iliyopita. 
  Hadi sasa Samatta amekwishaichezea Genk mechi 53 kwa Samatta tangu ajiunge na Genk Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya DRC akiwa amefunga mabao 18.
  Kati ya mechi hizo 53, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 34 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 32 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 22 msimu huu.
  Mechi 20 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 12 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 18, 12 amefunga msimu huu na sita msimu uliopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA KAZINI NA GENK YAKE LEO UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top