• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 21, 2017

  RASHFORD AIPELEKA MAN UNITED NUSU FAINALI ULAYA DAKIKA ZA NYONGEZA

  Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake, Anthony Martial na Michael Carrick baada ya kufunga bao la ushindi dakika ya 107 wakiilaza 2-1 Anderlecht katika mchezo wa marudiano robo Fainali michuano ya UEFA Europa League uliodumu kwa dakika 120 usiku wa Alhamisi Uwanja wa Old Trafford, Manchester baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika ya 90.
  Henrikh Mkhitaryan alianza kuifungia Man United dakika ya 10, kabla ya Sofiane Hanni kuisawazishia Anderlecht dakika ya 32 na kufanya sare ya jumla ya 2-2 baada ya timu hizo kutoa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Ubelgiji wiki iliyopita. Marcus Rashford akawa shujaa kwa kuifungia bao la ushindi United na kuipeleka Nusu Fainali PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RASHFORD AIPELEKA MAN UNITED NUSU FAINALI ULAYA DAKIKA ZA NYONGEZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top