MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amekosa penalti Real Madrid ikilazimishwa sare ya 2-2 na Valencia nyumbani katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Paco Alcacer alianza kuifungia Valencia dakika ya 20, kabla ya Javi Fuego kumtungua Iker Casillas kufunga la pili dakika sita baadaye.
Mkwaju wa penalti wa Cristiano Ronaldo ukaokolewa na kipa, Diego Alves kabla ya Pepe kuifungia Real bao la kwanza kwa kichwa akimalizia mpira wa kona dakika ya 56 na Isco kusawazisha dakika ya 84.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Arbeloa/Carvajal dk46, Pepe, Ramos, Coentrao/Marcelo dk46, Kroos/Illarramendi dk26, Ronaldo, James, Isco, Bale na Hernandez.
Valencia: Diego Alves, Barragan, Mustafi, Otamendi, Gaya, Fuego, Parejo, Gomes/De Paul dk78, Feghouli, Piatti/Orban dk90 na Alcacer/Negredo dk69
Cristiano Ronaldo akisikitika baada ya kukosa penalti katika mchezo ambao Real Madrid imelazimishwa sare ya 2-2 na Valencia PICHA ZAIDI GONGA HAPA


.png)
0 comments:
Post a Comment