URUGUAY imeanza vibaya Kombe la dunia baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Costa Rica usiku huu katika mchezo wa Kundi D Fortaleza, Brazil.
Uruguay ilitangulia kupata bao la penalti la Edinson Cavani dakika ya 24 kabla ya kinda wa Arsenal, Joe Campbell kuisawazishia Costa Rica dakika ya 54.
Huku mshambuliaji nyota wa Uruguay, Luis Suarez ambaye ni majeruhi akiwa benchi, alishuhudia jahazi la timu yake likizama kwa mabao mawili zadi kipindi cha pili.
Oscar Esau Duarte aliifungia Costa Rica bao dakika ya 57 kabla ya Marcos Urena kufunga la tatu dakika ya 84. Maxi Parera alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 90 na ushei kwa kumchezea rafu Campbell.
Haamini macho yake: Luis Suarez (kulia) akiwa benchi akishuhudia timu yake ikiadhiriwa
0 comments:
Post a Comment