MECHI zote 64 za Kombe la Dunia zitaonyeshwa kwenye ndege dunia nzima kwa mara ya kwanza kihistoria.
Dili hilo litafanyika kupitia channel ya Sport 24 itakayoonyesha mechi hizo kutoka Brazil, manna yake abiria hawatakuwa na wasiwasi wakiwa safarini watakosa mechi za timu zao.
Jumla ya mashirika tisa ya ndege yakiwemo Lufthansa, Emirates, Etihad ana Turkish Airlines yamesaini Mkataba huo.
Mechi nyingi zitaonyeshwa moja kwa moja wakati zinachezwa, ikiwemo ya ufunguzi wa mashindano baina ya wenyeji Brazil na Croatia Juni 12.
Picha za mechi zitachukuliwa na timu ya kampuni ya matangazo ya Televisheni ya FIFA, kabla ya kusafirishwa kwenye ndege na kampuni ya IMG Media.
Richard Wise, Rais Mkuu wa IMG Media, amesema: "Tumejifunga kuonyesha tukio hilo kubwa moja kwa moja kupitia Sport 24,".
0 comments:
Post a Comment