MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amerejesha matumaini Ureno kuelekea Kombe la Dunia baada ya kuanza tena mazoezi kufuatia kupata ahueni ya maumivu ya misuli yaliyokuwa yakimsumbua.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya misuli fulani kwenye mguu wake wa kushoto na kulikuwa kuna wasiwasi aneukosa mchezo wa kwanza wa Kombe la Dunia kati ya Ureno na Ujerumani Juni 16.
Pamoja na hayo, Chama cha Soka Ureno kimethibitisha kurejea kwa mchezaji huyo siku tisa kabla ya mchezo wao wa kwanza mjini Salvador.
Ronaldo akinyoosha misuli yake wakati wa mazoezi ya Ureno jana
Cristiano Ronaldo sasa anatarajiwa kucheza dhidi ya Ujerumani katika mchezo wa kwanza wa Ureno
0 comments:
Post a Comment