KAMPUNI ya usambazaji wa vifaa vya michezo, Puma itaisaida Arsenal kufanikisha mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Italia, Mario Balotelli kutoka AC Milan.
Mpachika mabao huyo anadhaminiwa na Puma, ambao pia mapema Januari walitanagza kuidhamini Arsenal.
Mustakabali wa Balotelli ndani ya Milan uko shakani baada ya Rais Silvio Berlusconi kusema bado hajaamua lolote kuhusu mchezaji huyo na mchambuzi wa Sky Sport nchini Italia, Mario Giunta akaandika: "Arsenal inamtaka sana Balotelli na Arsene Wenger atafanya kitu chochote kumhamishia London.
0 comments:
Post a Comment