UJERUMANI imeibuka na ushindi mono katika mchezo wa kirafiki na Armenia wa mabao 6-1 kujiandaa na Kombe la Dunia.
Ujerumani inayokwenda Brazil kupambana kumaliza ukame wa 18 bila taji la kimataifa, ilipata mabao yake tote kipindi cha pili.
Vifaa vya Ligi Kuu England: Mchezaji wa Chelsea, Andre Schuerrle aliifungia Ujerumani kwa krosi ya Lukas Podolski wa Arsenal
WAFUNGAJI BORA UJERUMANI DAIMA
MCHEZAJI | MABAO |
---|---|
Miroslav Klose | 69 |
Gerd Muller | 68 |
Jurgen Klinsmann | 47 |
Rudi Voller | 47 |
Lukas Podolski | 47 |
Karl-Heinz Rummenigge | 45 |
Mario Goetze alifunga mawili na Lukas Podolski, Andre Schuerrle, Benedikt Hoewedes ana Miroslav Klose kila mmoja akafunga moja.
Ujerumani ambayo imepangwa Kundi G pamoja na Ureno, Ghana na Marekani katika michuano hiyo inayoanza baadaye mwezi guu, ilicheza bila kipa wake chaguo la kwanza, Manuel Neuer ambaye anaendelea kupona taratibu maumivu ya bega.
Neuer, anayetarajiwa kuwa kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Kombe la Dunia dhidi ya Ureno, nafasi yake ilizibwa na kipa wa Borussia Dortmund, Roman Weidenfeller katika mechi ya pili mfululizo katika jana.
Klose sasa anakuwa mchezaji aliyeifungia mabao mengi zaidi Ujerumani, akifikisha mabao 69 na kumpiku gwiji, Gerd Muller mwenye mabao 68.
0 comments:
Post a Comment