BAO pekee la Oribe Peralta dakika ya 61 limeipa mwanzo mzuri Mexico baada ya kuilaza 1-0 Cameroon katika mchezo wa Kundi A Kombe la Dunia jioni hii Uwanja wa Dunas mjini Natal.
Refa wa Colombia, Wilmar Roldan alikataa mabao mawili ya Mexican akida mfungaji, mshambuliaji wa zamani wa Spurs, Giovani dos Santos alikuwa ameotea.
Matokeo hayo yanaiweka Mexico katika mazingira mazuri ya kufuzu sambamba na vinara wa kundi hilo, wenyeji Brazil ambao watamenyana nao Jumanne mjini Fortaleza.
Kikosi cha Mexico kilikuwa: Ochoa, Layun, Moreno, Marquez, Rodriguez, Aguilar, Guardado/Fabian dk69, Vazquez, Herrera, Giovani na Peralta/Hernandez dk74.
Cameroon: Itandje, Djeugoue/Nounkeu dk45, N'Koulou, Chedjou, Assou-Ekotto, Song/Webo dk79, Mbia, Enoh, Moukandjo, Eto'o na Choupo-Moting.
Kiboko yao: Peralta akishangilia baada ya kuifungia Mexico
0 comments:
Post a Comment