• HABARI MPYA

    Friday, October 18, 2013

    MICHUANO YA DK FENELLA MUKANGARA YAFIKIA PATAMU UBUNGO MSEWE

    Beki wa Amani FC, Kudura Kapacha, (kushoto) akiwania mpira na mshambuliaji wa Mbezi Unted, Sabri Twaha, katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu wa Kombe la Umoja na Amani mchezo uliofanyika Uwanja wa Ubungo Msewe, Dar es Salaam jana. Mbezi ilishinda 1-0. Michuano hiyo inaandaliwa na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Mh. DK Fenella Mukangara.


    Mshambuliaji wa Mbezi Unted, Ramadhani Athumani,kushoto akiwania mpira na Winga wa Amani FC, Cliff Philipo, kwenye  Ligi ya Umoja na Amani iliyofanyika Ubungo Msewe jijini Dar es Salaam. Mbezi ilishinda. 1-0


    Kipa wa Amani FC, Abdul Thomas, akijaribu kuokoa penati hiyo bila mafanikio wakati wa mchezo huo wa Ligi ya Umoja na Amani iliyofanyika Ubungo Msewe jijini Dar es Salaam. Mbezi ilishinda. 1-0



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHUANO YA DK FENELLA MUKANGARA YAFIKIA PATAMU UBUNGO MSEWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top