• HABARI MPYA

    Sunday, August 12, 2012

    USAIN BOLT AOMBA UKOCHA WA WASHAMBULIAJI MAN UNITED

    Usain Bolt
    USAIN BOLT amebeba Medali yake ya tatu ya Dhahabu na kumuambia Alex Ferguson: "Acha nikusadie kuwasimamisha Manchester City.
    Mtu huyo mwenye kasi zaidi duniani ameiambia The Sun anasali kuomba Manchester United wampe ofa ya kucheza Ligi Kuu.
    Lakini ikishindikana hivyo, Bolt anaomba hata apewe nafasi ya kuwanoa nyota wa timu hiyo kama Nani, Ashley Young na Antonio Valencia kwa sababu wako vizuri na wanaweza kuisimamisha City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu tena.
    Bolt, ambaye alibeba Medali yake ya tatu ya Dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki inayoendelea London, wakati Jamaica ikishinda mbio za 4x100 za relay, alisema: “Sijui kama Alex Ferguson atanipa ofa ya majaribio au hapana.
    “Lakini hata isiwe hivyo, ningependa kwenda kumsaidia kuwakochi washambuliaji wa United kama nilivyofanya kwa Ronaldo — nitafanya kila nitakachoweza kuhakikisha taji haliendi kwa Manchester City tena.
    “Unaona vijana kama Nani na Ashley Young ambao wana kasi na nguvu, lakini wanaondolewa kwenye mpira kama ilivyokuwa kwa Ronaldo pia.
    “Tangu nimfundishe Ronaldo mwaka 2009, sasa anafunga mabao 40 msimu mmoja, Sifikirii kama angeweza kufunga hivyo bila mafundisho yangu.
    “United ina wachezaji wengi wenye kasi ambao kama watapewa mbinu za kitaalamu za kukimbia itakuwa vigumu kukabiliana nao.
    “Wakati wowote, Alex Ferguson aniambie, nitafurahi kwenda kufanya kitu nilichofanya kwa Ronaldo, wale ni timu yangu.”alisema.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: USAIN BOLT AOMBA UKOCHA WA WASHAMBULIAJI MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top