• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 24, 2012

  'OKWI' APAGAWISHA MAZOEZINI YANGA


  Jioni ya leo, BIN ZUBEIRY alitembelea kambi ya mazoezi ya kikosi cha pili  cha Yanga, na kuwakuta wachezaji wa timu hiyo wakinolewa na makocha wao, wachezaji wa zamani wa timu hiyo, Salvatory Edward ‘Doctor’ na Abubakar Salum ‘Sure Boy’ Uwanja wa Kaunda, Dar es Salaam.
  Kivutio alikuwa ni kinda wa umri wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Msingi Lumumba, Suleiman Abdallah Kahera, maarufu kama Okwi mbele ya wachezaji wenzake akifananishwa na mshambuliaji wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi kiuchezaji. Dogo anayecheza wingi ya kushoto anajua na kama atapata malezi mazuri kisoka, miaka mitano ijayo, atakuwa habari nyingine. Ana kasi, uwezo wa kumiliki mpira, kuuchezea na kupiga chenga za kusisimua. Tazama picha za mazoezi hayo leo.
  Wachezaji wakisikiliza maelekezo ya walimu wao kulia


  Anayetabasamu kulia mbele ni Okwi wa Yanga B

  Makocha Salvatory Edward kulia na Sure Boy kushoto

  Mazoezi ya kuchezea mpira

  Dogo Okwi akifanya mambo

  Kocha Salvatory akiwafundisha kwa mifano

  Dogo Okwi kushoto ananyoosha viungo 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: 'OKWI' APAGAWISHA MAZOEZINI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top