• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 27, 2012

  MASHABIKI RWANDA WAGOMBEA JEZI ZA YANGA, ILIKUWA PATASHIKA ILE YA NGUO KUCHANIKA

  Mashabiki wa soka nchini Rwanda wameonyesha ni kiasi wanaipenda Yanga baada ya jana kugombana wakiwania jezi za klabu hiyo, iliyokuwa ziarani nchini humo. Patashika hiyo ya nguo kuchanika kuwania jezi za mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati ilitokea wakati wa mapumziko ya mchezo kati yao na Polisi, Uwanja wa Amahoro. Yanga ilikuwa Kigali tangu Jumanne iliyopita, kwa ziara ya michezo ya kirafiki na ikiwa huko, ilimtembelea rais Kagame Ikulu na pia kuzuru katika makaburi ya kumbukumbu ya mauaji ya Rwanda wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika mechi zake, Yanga, inayorejea leo Dar es Salaam iliifunga Rayon 2-0 Ijumaa na jana Polisi 2-1. Tazama picha hizi, zilizopigwa na Saleh Ally, Mhariri kiongozi gazeti la Championi jinsi watu walivyogombea jezi za Yanga.      • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASHABIKI RWANDA WAGOMBEA JEZI ZA YANGA, ILIKUWA PATASHIKA ILE YA NGUO KUCHANIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top