Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya


DZEKO KUTUA ARSENAL WALCOTT AKIHAMIA MANCHESTER CITY

Mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko, mwenye umri wa miaka 26, ghafala anatakiwa na Arsenal, katika dili la kubadilishana wachezaji, huku Theo Walcott akienda upande wa pili.
Hulk
Porto imekataa pauni Milioni 39.5 kumuuza Hulk
Porto imepiga chini dau la pauni Milioni 39.5 kutoka Zenit St Petersburg kwa mchezaji ambaye anatakiwa pia na Chelsea, Hulk, mwenye umri wa miaka 26.
West Ham itajaribu kwa mara ya mwisho kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili na kuwapa fursa Wekundu hao kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Theo Walcott.
Mshambuliaji wa Liverpool, Andy Carroll anajiandaa kuwa nje ya kikosi cha Wekundu hao kitakachocheza mechi ya Kombe la UEDA dhidi ya Hearts, habari zaidi zikisema ataondoka katika klabu hiyo.
Hamburg wamesema watafanya "lolote wawezalo" kukamilisha usajili wa kiungo wa Tottenham, Rafael van der Vaart, mwenye umri wa miaka 29, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Manchester City watapambana kukamilisha usajili beki wa Inter Milan, Maicon mwenye umri wa miaka 31, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Fulham imefeli mpango wa kumsajili kiungo Mark Noble wa West Ham, mwenye umri wa miaka 25 wakati wakitafuta mbadala wa Mousa Dembele ambaye amejiunga na Tottenham.
Scott Sinclair
Manchester City imeweka dau la pauni Milioni 6.2 kwa nyota wa Swansea, Scott Sinclair
Manchester City imeweka dau la pauni Milioni 6.2 kwa ajili ya winga wa Swansea, Scott Sinclair mwenye umri wa miaka 23.
Wakati huo huo, Swansea imekubali imekubali kutoa dau la rekodi la pauni Milioni 5.5 kwa ajili ua winga wa Valencia, Pablo Hernandez, mwenye umri wa mikaka 27, kama mbadala wa Sinclair.
Malaga inajiandaa kuipiga bao Real Betis katika mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Manchester City mwenye umri wa miaka 31, Roque Santa Cruz, kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania.

IRELAND KULA MAISHA VILLA

Stephen Ireland, mwenye umri wa miaka 26, anatarajia mkataba mpya kutoka Aston Villa, baada ya kuhakikishiwa maisha na kocha mpya, Paul Lambert.
Beki wa Chelsea, John Terry amesema kwamba yuko fiti kwa mechi za kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Moldova na Ukraine, baada ya kukosa mechi ya klabu yake, Chelsea dhidi ya Newcastle kwa sababu ya maumivu.